Katika tukio la aina yake, mwanamke mmoja raia wa Mali alijifungua watoto tisa kwa mpigo katika hali ambayo sio ya kawaida.
Halima Cisse mwenye umri wa miaka 25 alijifungua watoto wa kike watano na wavulana wanne katika hospitali moja nchini Morocco ambako alikuwa amelazwa mnamo mwezi Mei.
Hatua hiyo inajiri baada ya uvumi kwamba mwanamke mwengi nchini afrika Kusini alikuwa mejifungua watoto 10.
Hatahivyo habari hiyo haijathibitishwa na kwamba uchunguzi unaendelea.
Awali Bi Halima Cisse alitarajiwa kijifungua watoto saba kulingana na uchunguzi wa skani ya tumbo aliyofanyiwa nchini Mali na baadaye Morocco, lakini skani hiyo haikugundua kwamba amebeba watoto wengine wawili.
Wataalamu wanasema kuwa na mimba ya watoto wengi kwa mara moja hutokea iwapo tu kama mtu ametumia tiba ya uzazi.
Baada ya kusubiri kwa takribani miaka saba bila mtoto, Joyce Akhimien alijifungua watoto mapacha sita : watoto wavulana wanne na watoto wasichana wawili tarehe 12 Januari, 2021 huko Port Harcourt, Nigeria.
Hali ilikuwa vivyo hivyo kwa Doris Wilson mwenye miaka 49 yeye alisubiri miaka 21 na siku alipopata watoto Februari, 9 maka huu alipata watoto sita huko Nigeria.
Mimba nyingi zinazopelekea watu kujifungua watoto wengi , watoto wake huwa wanazaliwa kabla ya siku zao.
Sababu zinazopelekea mwanamke kuwa na mimba ya watoto wengi
Si jambo la kawaida kwa mwanamke kuzaa watoto zaidi ya watatu.
Lakini mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi Bill Kalumi, kutoka hospitali ya taifa ya Kenya amesema: “Mara nyingi hali hii hutokea iwapo mtu ametumia tiba ya uzazi.”
Ingawa kuna sababu inayowafanya watu kutafuta tiba ya uzazi.
Lakini hali hii hutokea sana barani Afrika wakati ambao mwanamke anaanza kutumia dawa za homoni ambazo ni kama za kuzuia kupata ujauzito.
Hii inaweza kumchukua muda kwa kipindi cha kutungwa mimba, Dkt Kalumi anaeleza.
Hivyo matokeo yake yanaweza kuwa mayai mengi badala ya moja wakati wa mzunguko wa mwanamke kwa mwezi.
Uzazi wa watoto wengi kwa pamoja, ni jambo la hatari kwa mama na watoto.
Mara nyingine baada ya kufanya vipimo vya picha, inashauriwa kupunguza idadi ya watoto waliopo tumboni.
CHANZO CHA PICHA,EPA
Na watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao yani kabla ya wiki 37, wako kwenye hatari ya kupata matatizo.
Watoto kuzaliwa wengi wako kwenye hatari ya kupata maambukizi.
Kwa muda mrefu watoto wanapozaliwa wengi, wanaweza kupata matatizo ya afya ambayo inaweza kusababisha matatizo ya kutembea.
Kwa huyu mama aliyejifungua watoto 10 hivi karibuni, Daktari anasema Sithole yupo kwenye hali nzuri.
Gosiame Thamara Sithole alidaiwa kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati mimba ikiwa na wiki 29 , huko Pretoria Jumatatu jioni.
Katika kitabu cha maajabu ya ulimwengu , cha Guiness book of world Records wamesema wanafanya utafiti juu ya kesi ya bi Sithole .
Mwanamke mwengine aliyejifungua watoto nane mwaka 2009 huko Marekani ndio anashikilia rekodi ya dunia ya Guiness kwa kujifungua watoto wengi kwa pamoja na wote kupona.
Dawa za kisasa tayari zinaruhusu wanawake kujifungua watoto umri ukiwa umeenda tofauti na wakati wa mababu zetu.