NA MCHANGA HAROUB-PEMBA.
Wanaharakati wa kupinga vitendo vya udhallishaji katika Mkoa wa Kusini Pemba wamesema changamoto kubwa katika kesi za udhalilishaji ni kukosekana kwa ushahidi kwani mashahidi wengi hawafiki mahakamani kutoa ushahidi kutokana na sababu mbali mbali..
Wamesema hayo huko katika ofisi za Tamwa Mkanjuni kisiwani Pemba katika mdahalo wa kujadili changamoto katika kesi za udhalilishaji.
Wamesema mashahidi wengi hawahudhuriimahakamani kwa madau ya kukosa fedha za nauli jambo ambalo husababisha kesi nyingi kufutwa kwa kukaa muda mrefu kwa kukosa ushahidi.
Akitoa ufafanunuzi juu ya kukosekana kwa fedha hizo mrajis wa mahakama Pemba Abdulrazak Abdul kadir, amekiri kuwa ni kweli fedha hizo hazitolewi na mahakama kwa wakati kutokana na ufinyu wa bajeti, na kueleza kwamba Serikali inalitambua hilo na tayari limeshaanza kufanyiwa kazi.
Aidha Mrajis huyo amesema katika kutatua tatizo la kukaa kesi za udhalilishaji mahakamani kwa muda mrefu tayari Serikali imetoa kibali cha ajira za mahakimu 13 kwa kuongeza nguvu katika kushughulikia kesi za udhalilishaji na kwa upande wa Pemba kuna mahakimu watano ambao watashughulikia kesi hizo.
KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI