Monday, November 25

VIDEO: SOS yakabidhi bima za afya kwa watoto wenye mahitaji maalum Dodo Pujini..

NA KHADIJA KOMBO- PEMBA.

Wazazi pamoja na walezi wametakiwa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya Afya mapema pindi wanapopatwa na tatizo la kiafya na kupatiwa matibabu kwa haraka ili kukinga athari zinazoweza kujitokeza .

Wito huo umetolewa na Daktari  dhamana Wilaya ya Chake Chake ( DMO ) Mohammed Ali Jape wakati alipokuwa akikabidhi kadi za bima za Afya kwa watoto wenye mahitaji maalum zilizotolewa na shirika la SOS huko Dodo Pujini katika Wilaya ya Mkoani.

Amesema Bima ya afya ni muhimu kwani inasaidia kupata huduma hizo kwa urahisi hivyo amewataka wazazi kuzitunza vizuri na kuzitumia kila wanapokwenda katika vituo vya afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kwa Upande wake Mratib wa Shirika la SOS Kisiwani Pemba  Gharib Abdalla Hamad  amesema lengo la SOS kukabidhi bima hizo kwa watoto wenye mahitaji maalum ni kuhakikisha wanatatua matatizo ya kiafya yanayowakabili watoto hao kulingana na hali zao kiuchumi.

Nao wazazi hao wamelishukuru shirika la SOS kwa kuwapatia bima hizo kwani zitaweza kusaidia katika kukwamua matatizo mbalimbali ya kiafya yanayowakabili watoto hao.

Jumla ya watoto 54 wenye mahitaji maalum katika shehi ya ya Dodo Pujini wamekabidhiwa kadi hizo.

KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI