TIMU za Ufaransa, Ujerumani na Ureno zimefuzu Hatua ya 16 Bora baada ya mechi zao za mwisho za Kundi F leo.
Ureno imamaliza kwa sare ya 2-2 na Ufaransa leo Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest, Hungary.
Mabao ya Ureno yote yamefungwa na Cristiano Ronaldo na yote kwa penalti dakika ya 30 na 60, wakati ya Ufaransa yamefungwa na 45’+2 K. Benzema yote, la kwanza kwa penalti pia dakika ya 45 na ushei na la pili dakika ya 47 akimalizia pasi ya Paul Pogba.
Nayo Ujerumani imelizimishwa sare ya 2-2 na Hungary Uwanja wa Venue Allianz Arena Jijini Munich.
Mabao ya Ujerumani yamefungwa na Kai Havertz 66′ na Leon Goretzka dakika ya 84, wakati ya Hungary yamefungwa na Ádám Szalai dakika ya 11 na András Schäfer dakika ya 68.
Ufaransa inamaliza kileleni na pointi zake tano, ikifuatiwa na Ujerumani pointi nne na zote zinafuzu 16 Bora, wakati Ureno iliyomaliza na pointi nne pia inafuzu kama Mshindi wa tatu Bora huku safari ya Hungary ikiishia hapa.
Timu nyingine zilizofuzu 16 Bora ni Wales, Denmark, Italia, Austria, Uholanzi, Jamhuri ya Czech, Ubelgiji, Croatia, Hispania, Uawisi, England, Sweden na Ukraine.
RATIBA YA HATUA YA 16 BORA EURO 2020
Juni 26: Wales v Denmark Saa 1:00 usiku
Italia v Austria Saa 4:00 usiku
Juni 27:
Uholanzi v Jamhuri ya Czech Saa 1:00 usiku
Ubelgiji v Ureno Saa 4:00 usiku
Juni 28:
Croatia v Hispania Saa 1:00 usiku
Ufaransa v Uswisi Saa 4:00 usiku
Juni 29:
England v Ujerumani Saa 1:00 usiku
Sweden v Ukraine Saa 4:00 usiku