Mke wa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib akiskiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Wajane Zanzibar ( ZAWIO)Tabia Makame katika hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la Ustaarabu wa Mwanamke Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mwanaharakati wa masuala ya kijamii Raya Hamad Mchere akielezea maana ya ustaarabu wa Mwanamke katika Kongamano hilo hafla iliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Mjasiriamali Chiku Marzouk Ali akielezea anavyofahamu maana ya Ustaarabu wa Mwanamke katika Kongamano linalohusu Ustaarabu wa Mwanamke huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mjasiriamali Isha Salim Hamad aliyevaa Mtandio (rangi Nyekundu ) akielezea anavyofahamu maana ya Ustaarabu wa Mwanamke katika Kongamano linalohusu Ustaarabu wa Mwanamke huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Baadhi ya Wajasiriamali wakifuatilia Kongamano la Ustaarabu wa Mwanamke katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Picha Na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Na Rahma Khamis / Maelezo.
Mke wa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib amewataka Wanawake Nchini Kujiendeleza kibiashara na kuacha utegemezi ili kujiinua kiuchumi.
Akifungua Kongamano la 3 la Ustaarabu wa Mwanamke katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar amesema Wanawake ndio dira ya maendeleo katika jamii hivyo yupo tayari kutoa mashirikiano ili kuleta maendeleo ya Wanawake.
Amesema Ustaarabu wa Mwanamke unajegwa na heshima,Uzalendo pamoja na uaminifu hivyo lazima wapambane ili kufikia malengo yao.
Akifafanuwa zaid kuhusu ustaarabu wa Mwanamke Mama Zainab amesema Wazanzibari wanaustaarabu wao katika malezi kwani wanawajibu wa kuutumia ustaarabu huo kwa lengo la kupata malezi bora kwa vizazi vijavyo.
Aidha amewaasa Wanawake wa Zanzibar kuachana na mambo yasiyoleta faida katika maisha yao na kujikita zaid katika shuhuli ambazo zitaleta tija ya maendeleo katika jamii ikiwemo ujasiriamali .
Akitoa Maana ya ustaarabu wa Mwanamke Mwanaharakati wa masuala ya kijamii Raya Hamad Mchere amesema Mwanamke awe na uwezo wa kufikiri kitu ambacho kina manufaa kwa jamii kwani baadhi yao hawafahamu majukumu yao.
Nao Wanafunzi waliopatiwa mafunzo katika Kongamano hilo wamesema kuwa wamejifunza kuondokana na utegemezi kwa kufanya kazi mbali mbali za kujiendeleza kiuchumi ikiwemo kutengeneza mikoba.
“Kiukweli tumejifunza mambo mengi sana ambayo tulikua hatuyajui na yanaweza kutupatia fursa za maendeleo na kujiendeleza kwa kupanua biashara zetu”. walisema Wanafunzi hao.
Hata hivyo wamewashauri Vijana wenzao kuacha kukaa Nyumbani na kutegemea ajira kutoka Serikalini nakuacha woga jambo ambalo hurudisha nyuma jitihada za kujikwamua kiuchumi .
Kongamano hilo la siku nne ambalo mada mbili zimejadiliwa ikiwemo Kujitambua na Afya ya Jamii lenye kauli mbiu isemayo “MWANAMKE KAMATA FURSA DUNIA INAKUSUBIRI”