Sunday, March 16

Mata Hari:Wengi walifiriki alikuwa mcheza densi kumbe alikuwa jasusi mkuu wa Hitler

Wengi walimuona kama mchezaji densi na mnenguaji hatari wa mauno .Alikuwa amejenga msururu wa wapenzi katika nyadhifa kubwa kubwa za serikali nyingi za bara Uropa.

Hakuna aliyemshuku Mata Hari -Jasusi maarufu sana wa kike ambaye sasa mengi kumhusu yamefichulia

Asubuhi ya 15 Oktoba 1917 gari la kijeshi la rangi ya kijivu liliondoka kwenye gereza la Saint-Lazare katikati mwa Paris. Ndani yake akifuatana na watawa wawili na wakili wake, alikuwa mwanamke wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 41 aliyevaa kanzu ndefu na kofia pana,.

Muongo mmoja mapema mwanamke huyu alikuwa na ameiteka mikononi miji mikuu ya Ulaya. Alikuwa jasusi maarufu wa kike katika kile kinachojulikana kwa kiingereza kama “femme fatale” na alitambulika kwa kucheza densi na wapenzi wake walikuwa ni pamoja na mawaziri, wafanyabiashara wakubwa na majenerali.

Police photo of Mata Hari

CHANZO CHA PICHA,MUSEUM OF FRIESLAND COLLECTION, LEEUWARDEN

Maelezo ya picha,Picha ya polisi ya Mata Hari siku aliyokamatwa

Lakini vikaja vita, na ulimwengu ukabadilika. Alidhani angeweza kuendelea kutumia njia zake za kike na urembo kuitawala Ulaya kama alivyozoea. Lakini sasa wanaume waliokuwa madarakani walitaka kitu zaidi ya ngono. Walitaka habari za kijasusi .Na hatua hiyo ilimaanisha kufanya upelelezi.

Huyu alikuwa Mata Hari, na alikuwa karibu kuuawa.

Kosa lake? Kuwa jasusi aliyelipwa na Wajerumani, akitoa siri kutoka kwa maafisa wa jeshi la Washirika ambao alilala nao, na kuzipitisha kwa waajiri wake, na kusababisha madai ya magazeti juu kwamba alihusika na kuuawa kwa maelfu ya wanajeshi wa Washirika .

Lakini ushahidi uliowasilishwa katika kesi yake, pamoja na nyaraka zingine, zinaangazia hali tofauti: kwamba kweli alikuwa jasusi wa pande zote mbili na huenda alikua ametolewa kama kafara .

Sasa, zaidi ya miaka mia moja baadaye, mwanga mpya umetolewa kuhusu jasusi mashuhuri zaidi mwanamke baada ya kufichuliwa kwa nyaraka za siri zilizotolewa na wizara ya ulinzi ya Ufaransa.

Hizi ni pamoja na nakala za kuhojiwa kwake na huduma ya upelelezi ya Ufaransa mnamo 1917. Nyingine pia zimeonyeshwa kwenye maonyesho mapya kwenye Jumba la kumbukumbu la Fries katika mji alikozaliwa wa Leeuwarden nchini Uholanzi.

Mata Hari's brooch

CHANZO CHA PICHA,ERIK AND PETRA HESMERG

Miongoni mwa majarida hayo ni ujumbe wa telegram kwenda Berlin kutoka kwa balozi wa kijeshi wa Berlin huko Madrid ambao ulisababisha kukamatwa kwa Mata Hari katika hoteli ya Champs-Elysees, na baadaye kutumika kama ushahidi muhimu katika kesi yake fupi.

Alizaliwa kwa jina Margarethe Zelle mnamo 1876, Mata Hari (jina linasemekana kutoka kwa lugha ya indonesia ‘jicho la siku’ – jua) alikuwa na maisha ya kushangaza na ya kutisha. Baada ya ndoa ya kusikitisha huko Mashariki mwa Indies alijifanya tena kama diva ya “Belle Epoque” Paris, ambapo densi zake za kimapenzi zilikuwa tiketi ya kuingia katika kilele cha jamii ya watu tajika huko Uropa.

“Hata bila tuhuma za ujasusi , Mata Hari angekumbukwa leo kwa sababu ya kile alichofanya katika miji mikuu ya Uropa mwanzoni mwa karne iliyopita,” anasema Hans Groeneweg, msimamizi wa Jumba la kumbukumbu la Fries.

“Alivumbua mtindo fulani wa kujivua nguo ukicheza muziki kama aina ya densi. Tuna picha na majarida ya michoro yake kwenye maonyesho, na kuna marundo na marundo ya vipande vya picha na picha za magazeti. Alikuwa mtu mashuhuri.”

Je alikuwa jasusi wa pande zote mbili?

Cha kusikitisha ni kwamba simulizi ya maisha ya Mata Hari inaongozwa na madai ya ujasusi. Kwa miaka mingi wanahistoria wengi wamemtetea. Alitolewa kafara – wengine wanasema – kwa sababu Wafaransa walihitaji kupata mpelelezi wa kumbandikia mfululizo wao wa kufaulu vitani baada ya kuonekana kushindwa hapo awali

Dutch dancer and spy Margaretha Geertruida Zelle, better-known as Mata Hari

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kwa wanaharakati wa kuwatetea wanawake, alikuwa kisingizio bora kwa sababu ‘upotofu wa maadili au mwanamke kuonekana kuwa “huru” yalifanya iwe rahisi kumchukulia kama adui wa Ufaransa.

Hadi sasa maelezo kamili ya kuhojiwa kwake na mwendesha mashtaka Pierre Bouchardon (kwa sadfa ndiye mtu ambaye baadaye alimshtaki Marshal Petain) yamekuwa marufuku kwa wanahistoria.

Ilijulikana, ingawa, mnamo 1916 – baada ya kukaa kwa muda mfupi huko London ambapo alihojiwa na huduma ya usalama ya Uingereza, MI5 – Mata Hari alirudi Ufaransa kupitia Uhispania.

Huko Madrid alifanya uarafiki wa Arnold von Kalle, balozi wa jeshi la Ujerumani. Maelezo yake ya baadaye ilikuwa kwamba hii yote ilikuwa kufuatia mpangilio wake wa mapema na huduama ya ujasusi ya Ufaransa, ambapo aliamua kutumia mtandao wake wa kabla ya vita na Ujerumani kusaidia juhudi za majeshi ya Washirika.

Lakini ilikuwa telegram iliyofuata ya von Kalle iliyosababisha kukamatwa kwake. Ndani yake aliwaeleza wakuu wake huko Berlin, maelezo ya ajenti fulani kwa jina H21. Maelezo hayo yalitoa anwani, maelezo ya benki, na hata jina la mjakazi mwaminifu wa Mata Hari. Hakuwezi kuwa na swali kwa mtu yeyote anayesoma kwamba Mata Hari alikuwa anjeti kwa jina H21.

Telegrafu, iliyozuiliwa na maafisa wa ujasusi wa Ufaransa, sasa inapatikana katika maonyesho ya Leeuwarden.Kulingana na wanahistoria wengine, sakata yote ya telegram hiyo ina hila

Huko Ufaransa – inasemekana – kwa muda mrefu kwamba Wafaransa walikuwa wameshang’amua kodi za siri za jumbe za telegram zilizoandikwa. Wajerumani walijua Wafaransa wameipasua kodi hiyo. Na bado von Kalle alituma ujumbe. Kwa njia nyingine, alitaka Wafaransa wasome.

Kwa hivyo, katika nadharia hii, Wajerumani ndio waliongoza Wafaransa kumkamata na kumuangamiza ajenti wao

Au kuna nadharia nyingine.

Kwa nini kuna tafsiri tu kwenye kumbukumbu? Ambapo swali ni iko wapi telegram asili? Inawezekana kwamba Wafaransa wenyewe walijitungia hati hiyo ili kumshtaki Mata Hari? Kwa njia hiyo wangepata “mpelelezi” wao. Na umma utaridhika.

Nadharia zote mbili zinamfanya Mata Hari kuwa mwathirika. Upande mmoja au mwingine uliona ni rahisi kumwondoa, na ndivyo walivyofanya.

Lakini nyaraka za Ufaransa zinatoa maelezo mengine, ambayo kwa kweli yanazipuuza nadharia hizo mbili .Kwa sababu maandishi ambayo yanaonyesha kwamba mnamo Juni 1917, wakati wa mahojiano yake ya kumi na moja, Margarethe Zelle aliamua kujitokeza wazi: alikiri.

Alimwambia Bouchardon kwamba ndio, alikuwa ameajiriwa na Wajerumani. Ilikuwa ni mnamo 1915 huko The Hague.

Kuuawa kwa Mata Hari

Alishikwa nje ya Ufaransa mwanzoni mwa vita, alikuwa na hamu ya kurudi Paris. Karl Kroemer, balozi wa Ujerumani huko Amsterdam, alimpa njia… ikiwa atakuwa mzuri sana kuwasaidia na habari fulani mara kwa mara. Kwa hivyo liliundwa jina la ajenti H21.

Mata Hari alisisitiza kwa wanaomuuliza maswali kuwa alitaka tu kuchukua pesa na kukimbia. Alisema uaminifu wake ulikuwa kwa Washirika, kama alivyoonyesha wakati baadaye aliahidi kusaidia ujasusi wa Ufaransa. Lakini ushahidi dhidi yake ulikuwa wazi sasa.

The French court's notification of Mata Hari's death sentence

CHANZO CHA PICHA,MUSEUM OF FRIESLAND COLLECTION, LEEUWARDEN

Maelezo ya picha,Arifa ya mahakama yaUfaransa kuhusu hukumu dhidi ya Mata Hari

Kufika Chateau de Vincennes nje kidogo ya mashariki mwa Paris, Mata Hari aliongozwa hadi kwenye kipande cha ardhi ambapo chapisho lilikuwa limewekwa. Wanajeshi kumi na wawili waliunda kikosi cha kufyatua risasi.

Ripoti zingine zinasema alikataa kufunikwa macho. Kamanda alishusha mikoni yake kwa mwendo wa haraka, na milio ya risasi ikasikiza – Mata Hari alianguka .

Afisa mmoja alikaribia na bastola na kumpiga risasi mara moja kichwani.

Baada ya kunyongwa, hakuna mtu aliyekuja kudai mwili wa Mata Hari. Kwa hivyo ulifikishwa kwa shule ya matibabu huko Paris ambapo ulitumika kwa masomo na utafiti. Kichwa chake kilihifadhiwa kwenye Jumba la kumbukumbu la Anatomia. Lakini miaka 20 iliyopita, iligundulika kuwa kimetoweka.Inadhaniwa kichwa chake kiliibiwa