Na Shaib Kifaya Pemba.
FAMILIA ya Amed Alfalas, kutoka Dubai akiongoza na wasaidizi wake Umewasili Kisiwani Pemba na kutembelea hospital tofauti kwa lengo la kuangalia Changamoto na kuzisaidia.
Hayo yamelezwa na Waziri wa afya Ustawi Wajamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar, Nasoor Ahmed Mazrou, wakati wa Ziara hiyo huko hospital ya Vitongoji Cottage.
Alisema lengo la Mfadhili huyo Armed Alfalas Kutoka Dubai ni kusaidia Vifaa tiba na mashine mbali mbali kwa hospital kwa vile ameona kuna mapungufu makubwa yanayohitajika wakati wa utoaji wa huduma kwa wananchi na kuahidi kujenga kituo cha Usafishaji damu cha Wagonjwa wenye matatizo ya Figo ili kuepuka gharama za kwenda Unguja kimatibabu pamoja na kuahidi kujenga jengo la mama na mtoto na kutoa mashine mbali mbali za uchunguzi kwa hospital za Pemba
” Kwa kweli kuja Ujumbe huu wa familia ya bwana Armed Alfalas imetupa matumaini makubwa kwetu Kwan ametuahid mambo mengi yenye mafanikio kwa maslahi ya wananchi wetu na serikali yetu “alisema Waziri Mazour
Nae Ahmed Alfalas kutoka Dubai, alisema lengo la Ziara kwa Visiwa viwili vya Unguja na Pemba, ni kutembelea hospital na kuangalia changamoto zilizomo na kuweza kusaidia.
Akizungumzia kwa Upande wa Pemba kwenye ziara hiyo alibaini kunamapungufu makubwa sana kwa hospital na kusema anategemea kujenga kituoa Kikubwa cha Uchunguzi wa damu kwa wagonjwa wanao sumbuliwa na maradhi ya figo ili kupunguza gharama za kwenda matibabu Unguja kutokana na hali zao kuwa duni pamoja na kuahid kujenga jengo la mama na mtoto hospital ya Cottage Vitongoji kutokana na uhaba wa nafasi kwa mama wajawazito.
Kwa Upande wake Afisa Mdhamini wa Wizara ya Afya Ustawi WA Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Yakoub Muhammed Shoka ,alisema kwa Upande wa serikali utahakikisha wanatoa mashirikiano na Ujumbe huo muda wote kwa yale ambayo ameahidi kuwasaidia.
Akitoa neno la shukurani kwa Ujumbe huo daktar dhamana wa hospital ya Cottage ya Vitongoji Sharif Hamad Khatibu alisema ziara ya Ahmed Alfalas, Kutok Dubai imewapa matumaini makubwa kwani ameahidi kuwapatia mashine na vya Uchunguzi na vifaa tiba ambavyo kwao ni muhimu sana kwa shughuli za utoaji wa huduma kwa jamii
Katika ziara yake hiyo Waziri na Ujumbe huo walitembelea hospital ya Cottage Vitongoji na Micheweni, Wete hospital .