NA ABDI SULEIMAN.
VIONGOZI wa Serikali Kisiwani Pemba, wamesema kuwa licha ya kisiwa hicho kuwa na bandari bubu nyingi, hivyo watahakikisha mkazo zaidi unawekwa katika maeneo hayo ili kudhibiti wimbi la tatu la Covid 19 kutokea.
Kisiwa cha Pemba kimejaaliwa kuwa na bandari bubu zaidi ya 300, hivyo mikakati hiyo ni pamoja na elimu kutolewa, kupimwa kwa afya wanaoingia nchini, pamoja na kuwekwa vifaa mbali mbali vya kukabiliana na wimbo hilo.
Viongozi hao waliyaeleza hayo katika kikao cha kuunda mkakati juu ya kujilinda na kujikinga na wimbo la tatu la Corovid 19, ambalo tayari limeashaanza kwa kasi na dalili zake kubadilika.
Akichangia katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Wete Mgeni Khatib Yahya, alisema mikakati zaidi inahitajika katika bandari bubu kuzuilika kutumika kuingia kwa wananchi kutoka nje ya Zanzibar.
“Lazima tuweke mikakati kuhakikisha bandari bubu hizi hazitatumika kuingia watu, Wilayah iii ya Micheweni inabandari nyingi sana”alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Kepteni Mstaafu wa KMKM Mohamed Mussa Seif alisema watendelea kuelimisha jamii kama ilivyokuwa katika COVIDI 19 awamu ya kwanza na pili, kwa kutumia mikakati waliokuwa nayo.
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake na kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Abdalla Rashid Ali, alisema watahakikisha katika mikutano yote ya karafuu kwa msimuu, pia wanazungumzia suala zima la kujikinga na wimbo la tatu la ugonjwa wa Covidi 19.
“Sisi viongozi ni wajibu wetu sasa kuwafahamisha masheha wetu wote, juu ya kuifikisha elimu hii ya Covidi 19 kwa wananchi zaidi vijijini, kwani huko ndiko elimu inakokosekana kufika”alisema.
Akiwasilisha mada katika mkutano huo, juu ya hali halisi ya Covidi 19 katika kisiwa cha Pemba, Mkuu wa tiba dhidi ya maradhi ya mripuko Pemba Dr.Aboud Khamis Maabadi, alisema katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2021, jumla ya washukiwa 49 walioibuliwa katika vituo na hospitali za Pemba, wanawake 22 na wanaume 27.
Alisema kutokana na uwepo wa viashiria vya hali ya hatari ya wimbo la tatu Covidi 19, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imeamua kuongoza nguvu juu ya tahadhari ya tahadhari ya kujikinga na maradhi ya Covidi 19, katika maeneo ya Bandarini/Viwanja vya Ndege, Hospitali na vituo vya afya.
Mapema akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Masoud Zahor, alisema wimbi la tatu la Covidi 19 limekuwa tafauti na wimbi la kwanza na la pili la maradhi hayo.
“Ipo haja ya kushusha taaluma kwa wananchi, zaidi ngazi ya nchini ili kuweza kujuwa athari na njia za kujikinga na uongojiwa huo hatari duniani”alisema.
Akizunguzmia juu ya suala la utumiaji wa barakoa, aliwashauri wananchi kutumia zaidi barakoa za kushona wenyewe kuliko barakoa za kununua kutoka nje ya nchi.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya uongonjwa huo, ambao tayari umeshapoteza maisha ya watu wengi duniani.
Naye mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, alisema kila kiongozi anapaswa kufuata muongozo wa kitaifa wa Covidi 19 katika kuchukua hatua, sambamba na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi hususan vijijini.
Afisa Mdhamini Wizara ya Afisa jinsia, ustawi wa jamii, wazee na watoto Pemba Yakub Mohamed Shoka alisema wimbi la tatu la Covidi 19, limekuja tafauti na wimbi zilizopita kutokana na dalili zake.
“Tumepita katika wimbi la kwanza, wimbi la pili tumefanya juhudi kubwa kwa kushirikiana na viongozi wetu wote, tulifanikiwa kwa asilimia kubwa, sasa mbili hili la tatu jitihada zaidi zinahitajika kuwekwa, hili dalili zake ziko tafauti na yaliyopita”alisema.
“Wimbi hili linakamata kila kundi ndio maana serikali tukaamua tukutane tuone jinsi gani tutaweza kukabiliana nalo na hatimae kuwanusuru wananchi wetu”aliongeza Mdhamini.
Hata hivyo alisema mikakati Mikubwa ni kusimamia suala zima la kukosha mikono kwa maji ya kutiririka, sabubi na pia kutumia sanitaiza, tunaishukuru serikali kwamba tuko vizuri katika hayo kwani vifaa vyote kwa hatua ya kwanza vipo katika stooo ya wizara.