Tuesday, November 26

VIDEO: Bidhaa zenye thamani ya zaidi ya shilingi 30,000,000 zimeangamizwa .

 

NA KHADIJA KOMBO –PEMBA.

Bidhaa mchanganyiko zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni thelathini (30,000,000) zilizoharibika zimeangamizwa kutokana na kuwa hazifai kwa matumizi ya binaadamu.

Akizungumzana katika kazi ya uangamizaji huko Pujini Mkurugenzi wa Idara ya kumlinda mlaji na udhibiti wa bidhaa bandia  Zanzibar Alya Emannuel Juma amesema bidhaa hizo zimekamatwa kutoka kwa wafanya biashara mbali mbali kutokana na ukaguzi wanaoufanya katika maduka na maghala ya wafanyabiashara hao.

Amesema baadhi ya bidhaa bado hazijapitiwa na wakati lakini kutokana na utunzaji mbaya wa bidhaa inasababisha kuharibika hivyo amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wana panga bidhaa zao vizuri ili zisiweze kuharibika.

Naye Ali Omar Masoud afisa kutoka Tume ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mtumiaji amesema matumizi ya bidhaa hizo zilizoharibika kunaweza kuleta athari mbali mbali za kiafya kwa mtumiaji.

Hivyo amewataka wananchi kuwa nat ahadhari juu ya bidhaa wanazonunua kwa kuangalia muda wa matumizi kwa bidhaa hizo.

Bidhaa zilizoangamizwa ni pamoja na tani 5 za mchele paket 177 za tende pamoja na bidhaa mchanganyiko kama  vile sabuni, biskuti na mafuta.

ANGALIA VIDEO HAPO CHINI