Inadaiwa kwamba inatumia akili bandia kuwatafutia wapenzi mabarobaro wanaotaka ndoa za kudumu na mke mmoja pekee.
Iran imezindua programu ya kuchumbiana inayolenga kuhakikisha kwamba kuna ndoa za kudumu katika taifa hilo la Kiislamu , ambapo viwango vya talaka vimeongezeka huku huku idadi ya Watoto wanaozaliwa ikipungua.
Hamdan , ikimaanisha mwenzako kwa lugha ya Persia , ilianzishwa na bodi ambayo ni miongoni mwa shirika la Propaganda la Kiislamu.
Inadaiwa kwamba inatumia akili bandia kuwatafutia wapenzi mabarobaro wanaotaka ndoa za kudumu na mke mmoja pekee.
Programu za kuchumbiana ni maarufu nchini Iran, lakini kwasasa ni programu ya Hamdan pekee itakayokuwa halali.
Sheria ya Iran inakataza uhusiano uliopo nje ya ndoa.
Kulingana na mtandao wa Hamdan, watumizi wake watalazimika kuthibitisha utambulisho wao na kufanyiwa vipimo vya kiakili kabla ya kuruhusiwa kutafuta mpenzi.
Wakati atakapopata mpenzi , programu hiyo itawaleta pamoja watu wa familia za wawili hao zikishirikiana na washauri wawili ambao wataandamana na wanandoa hao miaka minne baada ya ndoa hiyo.
Mkuu wa taasisi ya kitamaduni ya Tebyan Cultural Institute, ambayo iliunda programu hiyo anasema kwamba programu hiyo itajenga familia nzuri wakati ambapo thamani ya maadili ya kifamilia ipo hatarini kutoka kwa shetani na maadui wa Iran.
Kulingana na takwimu kutoka kwa Shirika la usajili wa raia , takriban ndoa 301,300 na talaka 99,000 zilirekodiwa nchini Iran kati ya Machi hadi Disemba 2020.
Mwaka 2008, kulikuwa na talaka moja katika kila ndoa nane.
Wakati huohuo ukuaji wa kiuchumi nchini Iran ulishuka hadi asilimia 1.29 mwaka 2020.
Zaidi ya nusu ya idadi hiyo ipo chini ya watu wenye umri wa miaka 35.
Lakini serikali imeonya kwamba iwapo hakuna hatua itachukuliwa huenda taifa hilo likawa miongoni mwa mataifa yenye wazee wengi katika miongo mitatu ijayo.
Mwezi Machi , bunge la Iran lilipitisha muswada unaoishurutisha serikali kutoa zawadi za kifedha katika ndoa na kwa wanandoa walio na zaidi ya watoto wawili. Hatahivyo haijaidhinishwa na baraza hilo.
Mwaka uliopita mamlaka ilianza kupunguza huduma za mpango wa uzazi katika hospitali za serikali hususan kama vile kukata miraja ya uzazi Vasectomy haipatikani tena na dawa za kujilinda dhidi ya kushika ujauzito zinapatiwa wanawake ambao afya zao zipo hatarini.