Saturday, October 19

Vijana wafundwa afya ya uzazi

IMEELEZWA kuwa zaidi ya vijana Milioni 3000 wanafariki kila siku kwa sababu ambazo zinaweza kuepukika, ikiwemo ajali, unyanyasaji, matatizo ya afya ya uzazi ikiwemo maradhi ya kujamiana na Ukimwi.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa maendeleo ya Vijana Zanzibar, Kutoka Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Mwanaidi Mohamed Ali wakati alipokuwa akziungumza na waandishi wa habri mara baada ya kufungua mafunzo ya siku nne juu ya Afysa ya Uzazi kwa vijana yaliyofanyika mjini Chake Chake.

Alisema vijana ndio watu wanaokumbana na changamoto nyingi katika masuala ya afya ya uzazi, kutokana na kukumbana na vishawishi vingi katika umri wao.

Alifahamisha kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwelewa vijana juu ya masuala ya afya ya uzazi kwa vijana, kutokana na kuwa ndio wanaokumbana na changamoto kubwa.

“Unajuwa vijana wanakumbana na mambo mengi katika kipindi cha kuanzia miaka 15 hadi 30, kipindi hiki ni kibaya kwao kama hatojituliza ndio tukaona tuwapatie elimu hii, iweze kuwasaidia na kujitambua kwao”alisema.

Aidha aliwataka vijana kuhakikisha wanajitunza na kutumia vizuri ujana wao, ili kuepuka kuingiza katika vishawishi na maradhi hatarishi na nyemelezi.

Akizungumiza suala la amani, Mkurugenzi Mwanaidi aliwataka vijana kutambua tahamani yao katika jamii, kuhakikisha wanakua viongozi wazuri wa utunzaji wa amani nchini.

“Amani ndio kila kitu kwa sasa bila ya amani tusingekuwa hivi, lazima tuheshimu na tuilinde kwa nguvu zote amani yetu, hii ni tunu pekee kwa Tanzania”alisema.

Kwa upande wake mratimu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Pemba Ali Mussa Bakari, alilishukuru shirika la UNFPA kwa kushirikiana nao katika kuwapatia vijana mafunzo mbali mbali ikiwemo afya ya uzazi.

Alisema lengo ni kuwajengea uwezo vijana katika kukabiliana na mazingira, pamoja na kujuwa afya ya uzazi kwani vijana wengi elimu hiyo wameikosa.

“Vijana munapaswa kuiyona jamii ndio kila kitu kwenu, ikiwemo kubadilika katika masuala yenu, hii elimu ya afya ya uzazi ni elimu ikiwa mutaifanyia kazi na kuwafikishia vijana wenzenu.

Akiwasilisha mada ya afya uzazi Nassor Kassim kutoka UMATI, alisema alisema suala la afya ya Uzazi kwa vijana inaendelea kuwa ni changamoto kwa jamii, iliyotuzunguka katika jangwa la sahara.

Alisema miongoni mwa changamoto ni ndoa za utotoni, mimba zisizozakutarajiwa, utoaji wa mimba, maambukizi ya VVU pamoja na kufanya mapenzi na tendo la ndoa bila ya kutumia kinga, huku wanawake ikielezwa kuwa ndio waathirika wakubwa.

Alisema taarifa zilizopo zinaeleza kuwa baadhi ya vijana wanatabia ya kujamiana wakiwa na umri mdogo, ambako hupelekea kupatikana mimba za utotoni,magonjwa ya zinaa hata maambukizi ya UKIMWI.