Thursday, January 16

WASDEC na ICT lub Mkoani Kisiwani Pemba wapewa mafunzo na UNESCO juu ya kutafuta masoko ya biashara zao kupitia simu janja.

NA ABDI SULEIMAN.

VIJANA wa WASDEC na ICT lub Mkoani Kisiwani Pemba, wamesema Elimu waliopewa na shirika la UNESCO juu ya kutafuta masoko ya biashara zao kupitia simu janja(smartphone) yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikuba na kufikia malengo ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya kasiwa cha Pemba.

Walisema kwa sasa ndoto zao zimeashaanza kutimia, kwani wataweza kuitumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara zao ili kupata wateja na kutambukila duniani.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika skuli ya Mohamed Juma Pindua, wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyotolewa na UNESCO juu ya kuwezeshwa kutumia simu janja za kidigitali, kwa wanawake ambao wako nje ya mfumo rasmi waelimu, katika kutafuta masoko ya bidhao zao kupitia mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa WASDEC na ICT Lub Warda Aliya Mohamed, alisema kwa kiasi kikubwa mafunzo yataweza kuwasaidia, kwani walikuwa akitangaza biashara zao mkoani tu, sasa wataweza kutangaza biashara zao hata nje ya Tanzania.

“UNESCO hawakuwahi kutufanyia mafunzo kama haya, hili ni jambo zuri na muhimu sana kwetu, tutaweza kutangaza biashara zetu kupitia simu hizo”alisema.

Adiaha liwataka vijana wenzake kuzitumia simu hizo kwa malengo yaliyokususidwa ili kuwa wajasiriamali au wafanyabiasha wa kisasa, katika kutangaza biashara zao.

Hata hivyo wamewataka wananchi kukaa mkao wakupokea bidhaa zao wanazotengeneza kupitia mitandao ya simu, ili kuona kama wamewiva kupitia mafunzo waliopatiwa.

Naye katibu jumuiya ya WASDEC Mgeni Mohd Ussi, alisema dunia kwa sasa ni mwendo wa kidigitali, kila kitu kinapatikana kupitia digitali hivyo wataweza kutangaza biashara zao kupitia mitandaoni.

Alisema watahakikisha wanapata mafanikio kupitia simu hizo, kwa kuanza kutangaza biashara zao kwa kutumia mitandao ya kijamii, pamoja na kujuwa sheria za mitandao ili kuepuka faini au adhabu wanazoweza kukumbana nazo.

Kwa upande wake Afisa mradi msaidizi wa kuwawezesha akinamama vijana na watoto baleghe ambao wako skuli na nje ya mfumo wa elimu kutoka shirika la UNESCO Tanzinia Justin Mori, alisema lengo ni kuwapatia taalumua na kuwajulisha vijana wanaofanya kazi nje ya mfumo kwa akielimu, namna ya kutumia vifaa vya kidigitali katika kukuza biashara zao na kutafuta masoko kupitia mitandao ya kijamii.

Alisema iwapo vijana hao wataweza kutumia ipasavyo mitandao hiyo, wataweza kutangaza bidhaa zao kwa kumakini mkubwa na kupata kutafuta masoko kupitia mitandao hiyo ya kijamii.

Justin aliwataka vijana hao, kufahamu matumizi sahihi matumizi ya simu pamoja na vifaa vya kidigitali vilivyomo ndani ya simu ili kukuza biashara zao kupitia masomo mtandao.

“Kuwapatiua simu hizi itakuwa ni vichecheo kwao, kuona simu hizi zinatumika ipaswavyo kuona biashara za mitandaoni kutoka kijijini zimeanza kuwafikia.

Mapema akifungua mafunzo hayo kaimu Mkurugenzi Baraza la Mji Mkoani Mohamed Faki Saleh, alisema Wilaya ya Mkoani ni miongoni mwa wilaya zilizokuwa na bahati sana katika shirika la UNESCO, ikiwemo kasulu, sengerema na ngorongoro waliopatiwa miradi hiyo.

Aliwataka vijana hao kuzichangamkia fursa wanazopatiwa za upendeleo, kwa lengo la kumkomboa mtoto wa kike kielimu na kimaisha, kwani dunia sasa ipo kiganjani hivyo matumizi ya simu janja zitaweza kuwasaidia sana katika biashara zao.

“Tusitake kujuwa kila kitu kilichomo ndani ya simu, vizuri kuchukua kile ambacho tunachofundishwa na sio mambo mengine ambayo hayafai”alisema.

Hata hivyo aliwataka kuthamini juhudi zao wanazozifanya ikiwemo ajira zao wanazozifanya, katika suala zima la ujasiriamali kwani linaweza kuwakomboa kimaisha.

Mradi huu unatekelezwa na shirika la coica shirika la umoja wa mataifa elimu tamaduni sayayansi (UNESCO) na unajumuisha vituo tano ambavyo ni mwambe, mizingani, uweleni, pindua na ICT lub vinazojishuhulisha na mafunzo ya ujasiriamali, kupamba kuchora kusoma kwa njia ya kidigitali na kushona.