NA ABDI SULEIMAN.
MBUNGE wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba Hamad Hassan Chande, amesema kukamilika kwa banda la vyumba vinne vya kusomea litaweza kupunguza idadi ya wanafunzi 120 hadi 50 kwa darasa moja kwa sasa.
Chande alisema kukamilika kwa banda hilo, litaweza kuwafanya wanafunzi kukaa na kusoma kwa utulivu mkubwa pamoja na kumsikiliza mwalimu kile anachokifundisha.
Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, aliyaeleza hayo kwenye hafla ya kukabidhi banda moja la skuli kwa uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba na kamati ya skuli ya msingi kangagani Wilaya ya Wete, lililojengwa na wadau wa maendeleo kupitia mbunge huyo.
Aidha aliwataka walimu kujitahidi sana katika kusomesha wanafunzi, ili darasa la sita waweze kufanya vyema katika masomo na mitahani yao ya taifa.
Alifahamisha kuwa wafadhili wao Comfort Aid Internalional na Nyota Foundation, jicho na matumaini yao yapo kangagani katika kuliona banda hilo linadunu na kupasisha wanafunzi wengi, ili kuwekeza majengo mengine katika jimbo la kojani.
“Hichi ni kipimo kizuri kwa walimu sasa ili tuendelea kujengewa mabanda mengine na wafadhili wetu, basi tuhakikishe tunalitunza na kupasisha wanafunzi wengi darasa la sita”
Hata hivyo aliwataka walimu na wanafunzi wa skuli hiyo, kuhakikisha wanalitunza na kulithamini, ili liweze kudumu kwa muda mrefu.
Akizungumza kwa niaba ya afisa mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Afisa elimu Mjumuisho Pemba Ali Khamis Kombo, alisema kukamilika kwa banda hilo litaweza kuondosha msongomano wa wanafunzi 120 hadi 130 kusoma darasa moja.
Aidha alishukuru wafadhali waliojenga jengo hilo wamechangia 70%, huku mbunge wa jimbo la Kojani akichangia 30%, ambapo kwa kiasi kikubwa wameseza kuwapunguzia mzigo WEMA katika mahitaji ya madarasa na madawati ya skuli.
“Leo sote mashajidi tunakabidhiwa banda hili pamoja na madawati yake, wanafunzi kazi yao ni kusoma tu sasa jukumu la kulinda na kutunza ni kamati na walimu wa skuli”alisema.
Hata hivyo aliwataka walimu na kamati kutambua kuwa, vijiji vingi bado vinatabu ya majengo ya skuli, hivyo vizuri wanakijiji cha Kangagani kulitunza jengo hilo.
Katibu wa kamati ya ujenzi wa skuli hiyo ambaye pia ni mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi Kangagani, Sada Bakar Hamad alimshukuru mbunge huyo kwa juhudi zake za kuwapatia jengo hilo, kwani skuli bado inawanafunzi wengi licha ya kuingia mikondo mbiwili.
Aidha Katibu huyo alisema kukabidhiwa kwa banda hilo, litaweza kupunguza msongomano wa wanafunzi wengi kusoma darasa moja na sasa walimu wataweza kufundisha kwa umakini mkubwa sana na wanafunzi mkufahamu mwalimu wao.
Hata hivyo aliwataka wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kusaidia majengo mengine, kwani skuli ya kangagani ni miongoni mwa skuli kongwe katika kisiwa cha Pemba.
“Skuli yetu inawanafunzi 1389, awali darasa moja likichukuwa wanafunzi 120 na sasa wanakaa 50 kwa darasa moja, baada ya kumalizika kwa ujenzi wake”alisema.
Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wananchi wenzake wa kangagani Khamis Nyange Makame (Profesa Gogo) waliahidi kulitunza na kulithamini jengo hilo, kwa kulisimamia jengo hilo kuendelea kubakia katika hadhi yake.
Nao baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita, wameahidi kuvitunza vifaa vya skuli hiyi wameahidi kuvilinda na kuvithamani vifaa vililomo ndani ya skuli hiyo.