Na Shaib kifaya Pemba.
Uwongozi wa Wizara ya afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na watoto Kiswani Pemba ,wamezishukuru taasi za nje na ndani ya nchi kwa kuwawezesha madaktar bingwa kufika Zanzibar kwa lengo la kutoa matibabu kwa wananchi wa Pemba.
Katika kufanikisha shughuli za uwendeshaji wa kambi za matibabu kwa hospital ya Wete na Chake madaktar hao waliweza kushirikiana na madaktar wazalendo na kufanikiwa zaidi kwenye utoaji wa huduma hizo kwa wananchi walopatiwa huduma hizo.
Hayo yalizungumzwa na afisa mdhamini wa Wizara hiyo dokta Yakoub Mohammed Shoka ,kwa wakati tofaut alipokuwa akiwa aga madaktar huko hospital ya Wete na Chake Chake.
Mdhamini huyo alisema madaktar hao waliweza kuwatibu wagonjwa mbali mbali na kuwafanyia upasuaji kwa wale walokua wana matatizo ya mifupa kwa watu wazima na kuwafanyia upasuaji watoto ambao walikua na kesi za mikojo ,pamoja na wale wenye ulemavu ambao unarekebishika.
” kwa kweli tunawashukuru madaktar hawa kwa kuwa na moyo wa uzalendo kwa kuwatibu wananchi wetu jambo ambalo limewakomboa kwani wamepunguza gharama za matibabu kwa serikali ingebidi pesa hizo zifanyike kuwasafirisha kuwapeleka nje ya nchi ama Muhimbili “.aslisema Dokta Shoka
Kwa Upande wake Afisa Uwendeshaji tiba Dokta Yussuf Hamad Iddi, alisema wananchi wengi waliweza kujitokeza kufanyiwa uchunguzi wamagonjwa mbali mbali na kuoatiwa matibabu na kuwataka kutumia fursa hizo pale wanapo kuja watalamu hao kwani wananchi wengi ni wanyonge hawana uwezo wa kujitibu kwa wakati.
Nae kiongozi wa timu hiyo ya madaktar hao Dokt Mohammed Zaky kutoka nchini Egypt mtalamu wa magonjwa ya mifupa alisema wamebain wananchi wengi wanamatatizo na kesi nyingi ni mifupa na kuishukuru serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Watendaji wa Wizara hiyo kwa mandalizi mazur na mashirikiano waliyowapatia na kuwahidi kurejea tena baada ya miezi sita ijayo kutoa matibabu kama hayo.
Akitoa neno la shukurani kwa madaktar hao kaimu daktar dhamana wa hospital ya chake chake, Abrahman Said Mselem, alisema kazi za utoaji wa huduma za matibabu zilienda vizur kwa zaidi ya kesi 50 za magonjwa ya mifupa wamefanyiwa wwnanchi kwa hospitali hiya na zaid ya kesi 29 za mikojo wamefanyiwa watoto
Madaktari hao kutoka falme za kiarabu zilitoa madaktar hao kutoka nchini huko ni Saudia Arabia, Sudan, na Egypt.