Friday, January 17

Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 03.08.2021: Kane, Haaland, Lukaku, Trippier, Messi, Ramsey, Asensio, Ward-Prowse

Manchester City wamepungukiwa na pauni milioni 40 kati ya pauni milioni 160 bei ambayo Tottenham inataka kumuuza mshambuliaji wa England Harry Kane, 27. (Star)

Chelsea hawajakata tamaa ya matumaini ya kusaini tena mkataba na msambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku,28, kutoka klabu ya Serie A ya Inter Milan. (Athletic, subscription required)

Barcelona wako tayari kutangaza rasmi mkataba mpya wa miaka mitano wa mshambuliaji Muargentina Lionel Messi mwenye umri wa miaka 34 katika siku zijazo. (Sport)

Lionel Messi

CHANZO CHA PICHA,BBC/TWITTER

Newcastle United wameuliza juu ya uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Juventus, 30, raia wa Wales Aaron Ramsey. (Goal)

Manchester United ina miezi 12 ya kumshawishi mshambuliaji wa Borussia Dortmund raia wa Norway Erling Braut Haaland kwamba ni klabu sahihi kwake. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye anasakwa na Chelsea na klabu nyingine, anatarajiwa kuhama katika msimu wa kiangazi wa mwaka 2022 wakati klabu zitakapoweza kuweka kipengele cha kumuachilia cha takriban pauni milioni 75 kwenye mkataba wake wa Dortmund. (Manchester Evening News)

Aston Villa wamewasilisha ofa ya pili kwa ajili ya kiungo wa kati wa Southampton, mwenye umri wa miaka 26-Muingereza James Ward-Prowse baada ya ofa ya awali ya pauni milioni 25 kukataliwa. (Mail)

James Word Prowse

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Leicester City, Leeds United na Everton wanashindana kumsaini winga wa Real Madrid Muhispania Marco Asensio, 25. (Fichajes – in Spanish)

Atletico Madrid wanajiandaa kwa uwezekano wa kumuuza mlinzi-Kieran Trippier mwenye umri wa miaka 30 kwa klabu ya Manchester United ili kujiandaa kumchukua mchezaji wa Roma- Alessandro Florenzi, 30, kama mbadala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (AS – in Spanish)

Sheffield United wako katika mazungumzo kwa ajili ya kuingia katika mkataba na kiungo wa kati wa kikosi cha zamani cha England cha vijana walio chini ya umri wa miaka 21 Ronaldo Vieira, 23, kutoka Sampdoria. (Mail)

Newcastle United wanaangalia uwezekano wa kuingia mkataba na kiungo wa kati Mfaransa Boubacar Kamara, 21, kutoka Marseille kwa takriban pauni milioni 10. (Mail)

Ronaldo Viera

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Meneja wa klabu ya Roma boss Jose Mourinho yuko makini kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Borussia Dortmund Mdenmark Thomas Delaney, 29, baada ya kushindwa kusaini mkataba na mchezaji wa kimataifa wa Uswizi Granit Xhaka, 28, fkutoka Arsenal. (Sun)

Tottenham wako katika mazungumzo ya awali na Wolves kuhusu kusaini mkataba na Conor Coady, huku meneja wa Spurs ,Nuno Espirito Santo akiwa makini kujumuika tena na mlinzi wa England 28-England kaskazini mwa London. (Football Insider)

Meneja wa Inter Milan Simone Inzaghi ameazimia kuendelea kumsaka kiungo wa safu ya nyuma-kushoto wa Chelsea Marcos Alonso,30. (Calciomercato – in Italian)

Matthew Hope

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Arsenal na Everton wamekuwa wakihusishwa na uhamisho wa mshambuliaji wa klabu ya Schalke, 20- Mmarekani Matthew Hoppe. (Star)

Mlinda lango wa Argentina Willy Caballero anahusishwa na taarifa za kurejea katika klabu ya Ligi ya Uhispania ya Malaga baada ya kuachiliwa na Chelsea msimu huu. (Marca – in Spanish)

Norwich City wameanza mazungumzo na Bournemouth juu ya kusaini mkataba na kiungo wa kati Mdenmark Philip Billing, 25. (Football Insider)

CHANZO CHA HABARI BBC