Saturday, January 18

Wana NGOs watakiwa kuwa wawazi katika utowaji wa maoni juu ya kuzifanyia marekebisho sheria mbali mbali zinazowasilishwa kwao.

NA ABDI SULEIMAN.

MWENYEKITI wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Khadija Shamte Mzee, amesema jumuiya zisizo za kiserikali zinapaswa kuitumia fursa waliyonayo kwa kuwa wawazi katika utowaji wa maoni yao, juu ya kuzifanyia marekebisho sheria mbali mbali zinazowasilishwa kwao, ili ziende na wakati na kuleta mabadiliko  pale zinapotekelezwa kwa vitendo.

Alisema jumuiya hizo zinafanya kazi katika sekta tafauti katika utoaji wa huduma kwa jamii na wao ndio wanao kutana na jamii mara kwa mara katika vijiji vyao kutaka kujua shuhuli zao ili kuzipatia ufumbuzi.

Mwenyekiti  Khadija  aliyasema hayo ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chake Chake, wakati akifungua mkutano wa kujadili mapitio ya rasimu ya sheria ya Jumuiya Zisizo za Kiserikali  Zanzibar  namba 6 ya mwaka 1995, uliowashirikisha jumuiya za kiraia na kuandaliwa na jumuiya ya  PACSO kwa ufadhili wa jumuiya  ya PACT Tanzania.

Alisema  NGOs hizo zinafanya kazi kuribu sana na jamii kwenye utowaji wa huduma katika sekta mbali mbali, hivyo fursa kama hizo wanapaswa kuitumia kwa kutowa maoni yao kwa kuiangalia jamii zaidi kwani wao ndio wanao zifahamu shida zao.

Alifahamisha kuwa mipango ya kimaendeleo inayopangwa na serikali nil azima kuwe na NGOs kwa mahitaji makubwa ni kuihudumiakia jamii katika sekta tafauti.

“NGOs ni muhimu katika maendeleo ya nchi, kwa kuwasaidia wananchi waliochini ambao wao sauti zao hazisikiki kwa serikali,  ili kuona wananufaika kupitia jumuiya hizo” alisema.

Mapema Mrajis wa Jumuiya Zisizo za Kiserikali  Zanzibar Ahmed Khalid Abdalla, alisema kukamilika kwa sheria hiyo itaongeza kasi ya uwajibikaji na kuleta mabadiliko ya haraka ya maendeleo katika jamii.

Alisema serikali ya SMZ inajali na kuthamini juhudi zinazofanywa na NGOs, kwani lengo la serikali na  NGOs ni kuwatumikia wananchi katika suala zima  la kimaendeleo.

“NGOs  za  Pemba zimeonyesha nia kubuni miradi mikubwa na kufanikiwa, katika kipindi hiki kifupi tutashuhudia jumuiya za kimataifa kuja kuekeza  Zanzibar kwenye mambo mbalimbali”alisema.

Hata hivyo alizitaka Jumuiya kuhakikisha zinafuata sheria na  sera, katika utekelezaji wake wa majukumu yao huku akiipongeza  PACSO kwa kuendelea kuziunga mkono jumuiya  changa.

Akiwasilisha mada kuhusu mapitio ya sheria ya Jumuiya namba 6 ya Mwaka 1995, katibu wa tume ya kurekebisha sheria  Zanzibar  Mussa Kombo, alisema tokea mwaka 2009 sera ilitaka kuwepo kwa sheria mpya ya NGOS, kwani lengo ni kuondosha mapungufu yaliyo kuwepo katika suala zima la usajili.

Wakitoa maoni yao washiriki wa mkutano huo walizitaka taasisi za serikali kuacha kuziona NGOs  kama adui wao mkubwa,  bali zinapaswa kushirikiana na  NGOs katika suala la maendeleo.

Alisema kuna baadhi ya  NGOs zimekuwa zikifanya kazi kubwa ya kusaidiaj amii, ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, mabanda ya skuli,  uchimbaji wa visima vya maji, hivyo watendaji wanapaswa kuziunga mkono jumuiya hizo.