Thursday, January 16

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 04.08.2021: Maddison, Kane, Lukaku, Abraham, Ibrahimovic, Coady, Kounde

Manchester City wako tayari kulipa pauni milioni 130 kwa ajili ya mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27, na wamesalia kuwa na matumaini kwamba wanaweza kusaini mkataba naye. (Athletic, subscription required)

Arsenal wamependekeza mkataba wa nyongeza ya pesa kwa ajili ya kiungo wa kati wa Leicester City na England James Maddison.

Inasemekana The Gunners wanasita kulipa pauni milioni 60, malipo yanayotakikana kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, kwa hiyo watatoa ofa ya mchezaji kama sehemu ya dau hilo. (football.london)

 

KIungo wa kati wa klabu ya leicester City James Maddison
Maelezo ya picha,KIungo wa kati wa klabu ya leicester City James Maddison

Inter Milan watakubali kwa shingo upande dau la takriban pauni milioni 100 kutoka kwa mshambuliaji wa Chelsea Mbelgiji Romelu Lukaku, 28, baada ya maafisa katika klabu hiyo kukubali kibinafsi kuwa wanahitaji kumtoa mmoja wa wachezaji mashuhuri msimu huu ili kuweka sawa mahesabu yao ya pesa. (Metro)

Lukaku anasemekana kutaka kurejea Chelsea lakinii anahisi kuna mambo ambayo hajayajakamilika katika Stamford Bridge. (Sun)

Mlinzi wa Uhispania Aymeric Laporte ameieleza wazi Manchester City kwamba anahitaji kuhamia La Liga msimu huu, huku Barcelona na Real Madrid zikiwa makini kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (90min)

Aymeric Laporte

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Southampton na West Ham zinamtaka mlinzi wa kikosi cha vijana wenye umri wa miaka 21 wa Nice na Austria-21 Flavius Daniliuc, 20. (Mail)

Liverpool, pamoja na timu zisizojulikana za Primia ligi, wanataka kusaini mkataba na mshambuliajii wa Bournemouth Mholanzi Arnaut Danjuma, 24, ambaye tayari anatakiwa kwa dau na timu ya Villarreal. The Cherries wanasemekana kumtaka kwa mkataba huru wa pauni milioni 21.5. (Marca – in Spanish)

Aston Villa wana matumaini ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 23, na mlinzi wa Manchester United Axel Tuanzebe, 23. Wote walicheza kwa mkataba wa mkopo katika klabu ya Villa Park na waliisaidia klabu hiyo kupandishwa daraja na kuingia katika Primia Ligi katika 2018-19. (Telegraph – subscription required)

Chelsea wamemtoa kama ofa winga Mbrazili Kenedy kwa klabu ya Sevilla ikiwa ni kama sehemu ya mkataba wao na Jules Kounde,22, baada ya mlinzi mwenzake Mfaransa Kurt Zouma, 26, kutolewa awali katika sehemu ya kubadilishana wachezaji na the Blues. (Sun)

Christiano Ronaldo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo atataka bado kuondoka Juventus kuelekea Real Madrid, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, anafahamu kuwa fursa zake za kurejea Bernabeu zinategemea iwapo klabu hiyo ya Uhispania itafanikiwa katika harakati zake za kumtaka mshambuliaji wa Paris St-Germain, 22 Mfaransa Kylian Mbappe. (AS – in Spanish)

Wageni wa Primia Ligi Brentford wanakamilisha mkataba kwa ajili ya kiungo wa kati wa Midtjylland Msweden Swedenn 21, Jens Cajuste, ambaye amehusishwa na taarifa za kuhamia katika klabu ya Rennes. (Sportbladet – in Swedish)

Mshambuliaji Msweden Zlatan Ibrahimovic, 39, “alijaribu bahati yake” kuhusu uwezekano wa kurejea Paris St-Germain kabla ya kukubali mkataba mpya wa mwaka mmoja katika AC Milan. (Le Parisien – in French)

Leeds United wana ushindani katika dau la kusaini mkataba na mchezaji wa kikosi cha vijana walio china ya umri wa miaka 21 cha Uholanzi Noa Lang. Kulingana na ripoti klabu ya ligi ya Uhispania Sevilla pia wanamtaka winga huyo mwenye umri wa miaka 22. (El Desmarque – in Spanish)

Jesse Lingard

West Ham wanaamini wana asilimia 10 pekee ya uwezekano wa kusaini tena mkataba na mchezaji wa kimataifa wa England Jesse Lingard kutoka Manchester United. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye mkataba wake katika Old Trafford unaisha msimu ujao wa kiangazi, amerejea katika mazoezi kabla ya msimu na The Red Devils. (Sky Sports)

West Brom wanaangalia uwezekano wa kumhamisha mshambuliaji wa klabu ya Derby County kutoka Wales Tom Lawrence mwenye umri wa miaka 27. (Mail)

CHANZO CHA HABARI BBC.