Sunday, October 20

Zantel wawasogezea huduma wateja Wete.

MENEJA wa huduma kwa wateja wa Zantel, Fatma Mohammed Khalfan akizungumza na waandishi wa Habari wakati uzinduzi wa duka jipya la Zantel lilipo mjini Wete eneo la Four Ways, Kulia ni Said Masoud Ali, Meneja wa Mauzo na usambazaji Pemba, Duka hilo litarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

KATIKA kuhakikisha huduma za mawasiliano zinakuwa za uhakika, nchini Kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania, Zantel imezindua duka jipya la simu katika mji wa Wete kwa lengo la kurahisisha huduma zaidi kwa wananchi wa mji huo.

Duka hilo jimpya limekuja kufuatia duka la zamani lililoko Sokoni Wete, kutokukudhi mahitaji ya utoaji wa huduma kwa wateja kutokana na mabadiliko ya Teknolojia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkuu wa Masoko na Huduma za Kifedha wa Zantel, Sakyi Opoku alisema uwepo wa duka hilo utapunguza adha mbalimbali ambazo wateja walikumbana nazo awali.

Alisema uboreshaji wa duka hilo ni sehemu ya mkakati wa kampuni, wa kuhakikisha unasogeza huduma karibu na wateja ili kuhakikisha wanapata huduma na bidhaa za kampuni hiyo kwa urahisi.

“Hili duka tumelileta hapa makunao ya barabara za wete, ili wateja wetu wapate huduma kwa urahisi sana, huduma muhimu zote zinapatikana humu, pia munakituo cha kituo cha huduma kwa wateja kilichoboreshwa zaidi”alisema.

Aidha alisema Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar, kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.

Alifahamisha kwamba huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania, kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, mara baada ya uzinduzi wa duka hilo Meneja wa masoko na mawasiliano kutoka kampuni ya Zantel Rukia Mtingwa, alisema Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable.

Alisema mtandao huo ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani, umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.

“Hapa kwa siku kati ya watu 10 hadi 15 wataweza kupata huduma kwa wakati mmoja, kuwepo hapa tutaweza kuongeza wigo kwa watumiaji wa mtandao huu”alisema.

Kwa upande wake Fatma Mohamed Khalfan, alisema duka hilo linatarajiwa kuhudumia zaidi ya wateja 100, pamoja na kutoa huduma mbali mbali, ikiwamo usajili wa simu, huduma za kifedha (Ezypesa) na uuzaji wa simu mbalimbali zenye uwezo wa 4G ikiwamo simu aina ya Smarta.

Meneja wa Maduka ya Zantel Zanzibar Mwajuma Hussein, alisema duka hilo limetengenezwa kuhakikisha wateja wanapata huduma bora, zaikiwamo mfumo wa kidigitali kwa kusajili wateja badala ya kutumia foleni, ili kufanya huduma kuwa rahisi na haraka.

MENEJA wa Maduka ya Zantel-Zanzibar,Mwajuma Hussein akionesha namna ya kutumia mfumo wa utoaji tiketi kwa wateja (Cueing System) utakaorahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja

Mwakilishi kutoka PBZ bank Wete Bkari Ali Bakari, aliiutaka uongozi wa Zantel kuhakikisha wanaongeza nguvu katika mtandao wa Internet, kwani ndio wananchi wengi wamekuwa wakifurahia huduma zake.

Alisema changamoto kubwa inayowakumba wananchi na kuwa chini kwa huduma ya mtandao huo, hupelekea wananchi kuhamia mitandao mengine jambo ambalo wananchi hupiga kelele.