Sunday, October 20

Riziki haina mja wajipanga kuzalisha vitunguu maji.

 

KIKUNDI cha Riziki haina mja kinachojishuhulisha na kilimo mchanganyiko, kimesema kuwa baada ya kinakusudia kuendelea na kilimo cha vitunguu maji baada ya kuona zao hilo linakuwa katika eneo lao.

Kikundi hicho kinachotumia eneo la Mjini Ole makaani kwa shuhuli zake za kilimo, msimu huu kimeweza kupata kilo 127 za kitunguu maji zikiwa na thamani ya shilingi Milioni 1.2.

Akitoa taarifa ya kilimo hicho, msimamizi wa kilimo cha Vitunguu Maji katika kikundi hicho, Hamad Khamis Mussa alisema kilimo hicho kilikubali vizuri, ila kilikumbana na changamoto ya mvua wakati wakuvuna na kupelekea vitunguu vingi kuharibika.

“Kwa kiasi kikubwa hili zao linakubali katika eneo letu, awamu hii tumelima na tumeona mafanikio tulioyapata kutokana na mafanikio haya tutaongeza juhudi katika kilimo hiki”alisema.

Kwa upande washuhuli zakilimo cha Tungule, msimamizi wa kilimo hicho Omar Hamad Aminia alisema licha ya green House mmoja kupasuka na kuharibika kwa tungule ambazo zilikuwa tayari zimeshakaribia kuvunwa na kutokufikia malengo yao.

Alisema waliweza kuuza kiasi cha shilingi ilioni 1622000/=, na baada ya kutumia kwa maandalizi ya msimu mpya shilingi laki sita (600,000/=)zimebakia benk ikiwa ni faida.

Hata hivyo Omra alisema kwa sasa mikakati yao ni kuendelea na vilimo vyao, pamoja na kuingia katika ufugaji wa kuku wa kienyeji katika kikundi chao

Kwa upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba, Fatma Hamad Rajab aliutaka uongozi wa kikundi cha Riziki haina mja kuzidisha juhudi katika kufikia malengo yao walioyakusidia.

“Mafanikio makubwa mumeyapata hichi ni kukundi cha kutilia mfano, sasa jambo la kukata tama hapa lisikuwepo katika maisha yenu neema iko njiani itajitokeza tu”alisema.

Alisema kutokana na kasi ya Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi, itafika wakati hamutohitaji ajira yoyote kutoka serikalini, kutokana mikakati madhubuti iliyoweka katika kuwasaidia vijana.

Aidha alikuahidi kikundi hicho kukusaidia kupata mradi wa ufugaji wa kuku wakienyeji, ili kuweza kufikia maendeleo ya kiuchumi, ili ifike wakati vijana waweze kufika na kujifunza kutoka kwao.

Aliongez akuwa kisiwa cha Pemba kimejaaliwa kuw ana rutba nyingi, huku kikikubali kilimo cha aina yoyote kinachopandwa kinaota.

Hata hivyo aliwataka kuthamini juhudi zao wanazozitumia, pamoja na kuthamini mali za serikali wanazopatiwa na kuzitumia kwa malengo husika.

Afisa utumishi wa Wizara hiyo Mohamed Kombo (kimadi)alisema kikundi cha Riziki haina mja ni moja ya vikundi vya mfano katika kisiwa cha Pemba kwa sasa, kutokana na mikakati na maendeleo waliofikiwa.

“Kutokana na hali hii inavyokwenda na juhudi zenu, pamoja na ubunifu wenu ifike wakati kikundi hichi kiwe na chuo kwa vijana wengine kuja kujifunza kwenu”alisema.

Hata hivyo aliwataka kuongeza juhudi katika shuhuli zao, kwani serikali ya awamu ya nane imedhamiria kuwakombo vijana na kuwainua kimaisha.

Mratib wa idara ya maendeleo ya Vijana Pemba Ali Mussa Bakari, alisema kikundi hicho kimekuwa ni kikundi cha mfano, hivyo kutokana na mabadiliko ya serikali vijana wanatakio kujiongeza katika ubunifu wa kilimo.

Akizungumzia lengo la program ya ajira kwa vijana alisema ifike wakati kila mtu aweze kupata haki yake, kutokana na kilimo wanachozalisha.