(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
NA ABDI SULEIMAN.
WAZIRI wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulidi Mwita, amewataka wasanii wa vikundi vya sanaa Ksiiwani Pemba, kuhakikisha sanaa hiyo wanawarithisha vijana wao ili iweze kuendelea kudumu.
Alisema sanaa nyingi zimekua zikipotea kutokana na wazee kushindwa kuzirithisha kwa vijana wao, jambo ambalo linapelekea sanaa hizo kupotea siku hadi siku.
Waziri Tabia aliyaeleza hayo katika hutuba yake wakati wa mashindano ya vikundi vya sanaa Pemba, yaliyofanyika uwanja wa Michezo Gombani Chake Chake Pemba.
Aidha alisema Wizara itahakikisha inakamilisha yale yote yanayohitajika katika kuboresha sana za utamaduni zikiwemo ngoma za asili, ili ziweze kuendelea kubaki katika asili yake na kurisishwa kwa vizazi vya sasa vilivyopo bila ya kupoteza asilia yake.
“Tayari sisi kama Wizara tumeshaanza kuchukua hatua za kuviboresha vikundi mbali mbali vya sana, kwa kuanda matamasha na mashindano na matamasha mbali mbali ya asili”alisema.
Hata hivyo alisema wizara itaendelea kuimarisha kitengo cha haki miliki, ili wasanii waweze kupata haki zao wale ambao wataweza kuzisajili sanaa zao.
Naye Katibu mkuu wa wizara ya habari utamaduni na michezo Fatama Hamad Rajab, alisema Wizara imejipanga kuleta mabadiliko makubwa katika sana, hivyo aliwataka wasani kutoa mashirikiano yao ili kufanikisha malengo ya wizara ya kuboresha sana.
Kwa upande wake Mmoja wa waandaaji wa mashindano hayo Ibrahim Bukenga, ameitaka wizara kuhakikisha inawasimamia wasanii katika kulinda utamaduni wa mzanzibari amboa ndio urithi wa Zanzibar.
“Sanaa inapotumika katika majukwaa mbali mbali inatoa alama kubwa kwa taifa nan chi, hivyo ipo haja wasanii wetu kuendelea kuutangaza utamaduni wa mzanzibar na kutokuharibu”alisema.
Akitoa neno la shukurani kwa niamba ya vikundi vya sana Msanii Mohammed Kombo(mwenyi mpeku) aliutaka uongozi wa wizara, kukaa pamoja na vikundi vya sana kisiwani Pemba, ili kushirikiana katika kuboresha sana ikiwemo ya ngoma za utamaduni na sana za maonyesho.