NA ABDI SULEIMAN.
MTOTO wa kiume mwenye umri wa miaka 12, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi Chwale Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, amenusurika kufa baada ya kumeza vidonge 21 aina paracentamo (Panadoli), huku sababu za mtoto huyo kufanya maamuzi hayo baod hazijafahamika.
Taarifa za mtoto huyo kumeza vidonge zilianza kuzagaa katika maeneo ya mji wa Wete na kufunga safari hadi katika Hospitali ya Wete, alipokua amelazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, baadhi ya Walezi wa mtoto huyo pamoja na majirani jinsi tukio lilivyotokea na hatua zilizochukuliwa baada ya kumeza vidonge hivyo.
Fatama Ali Makame Mama mlezi wa mtoto huyo, alisema ilikuwa asubuhi alipokwenda mazikoni Mchangamdogo, aliporudi alipata taarifa kutoka kwa rafiki yake kuwa Ali ameshakula dawa.
“Mimi nilipomtafuta na nikamkuta kwenye goto lao amelala kila nikimwita hasemi kitu ananitizama ndipo nilipomwita baba yake mlezi na kuja tukampeleka spitali”alisema.
Naye baba mzazi wa Mtoto huyo Hamad Khamis Sheha, alisema tukio lilipotokea alikua sokoni na mtoto alikuwa ameshameza vidongo, hali ilikuwa mbaya na kumpatia maziwa kwa hatua ya kwanza na kumkimbiza spitali.
Kwa upande wake mwathirika wa tukio hilo alisema vidongo hivyo alinunua dukani kwa Pesa yake mwenyewe, wala hakuhimizwa au kulazimishwa na mtu.
Naye jirani wa mtoto huyo Zuweza Salim Ali aliwataka wazazi kukaa karibu na watoto wao karibu na kutokuwapatia au kuwatolea maneno makali, ambayo yanaweza kuwanyima na kuwafanya wakachukua maamuzi magumu.
“Watoto sio vizuri nao kuchukua maamuzi magumu wanapaswa kuwaeleza watu wao wa karibu juu ya matukio yote yanayowasibu wakati wanapokua majumbani mwano”alisema.
Daktari wa zamu wodi ya watoto hospitali ya Wete Khamis Juma Makame, alisema mtoto huyo alipokelewa akiwa katika hali mbaya kiafya na sasa hali yake inaendelea vizuri.
Dkt. Khamis alisema mtoto huyo walimpokea jioni, hakua katika hali nzuri na tulimpatia matibabu ya kwanza, chanzo halisi cha kula dawa hakijajulikana.
“Anavoonekana mtoto hana matatizo ya akili kwa ujumla, lakini kitaalamu inakua inatokea kuwa na matatizo ya akili kwa muda mfupi, daktari wa akili amezania amepata shida hiyo na kufanya kama alivyofanya”alisema.
Aidha alisema shira ya matatizo ya akili katika familia yao hakuna tatizo hilo, huku akiwataka wazazi kuhakikisha wanakuwa makini na watoto wao.
Kwa upande wake kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kamishna Msaidizi Jerome Felex ambaye amekiri kutokea tukio hilo sambamba na kuwataka wazazi kuwa makini na watoto wao.
Alisema mtoto huyo analelewa na shengazi yake kutoka kwa mama yake, lakini mtoto huyo inaelezwa alikuwa mtundu sana hataki kwenda skuli, aliitaka jamii kutambua kuwa mmomonyoko wa maadili umekua sana ni jukumu kuhakikisha wanakuwa makini na watoto wao.
Hata hivyo kamishna Msaidizi Jerome aliwataka wazazi kuhakikisha wanalea watoto wakapokua hai na sio kuwapeleka kwa wanafamilia wengine kama iliyokuwa kwa mtoto huyo.