Monday, November 25

VIDEO: Skuli ya Wesha yakabidhiwa Tsh milioni 9,000,000/=.

Na Raya Ahmada-Pemba.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh. Lela Mohamed Mussa amesema ubovu wa madarasa matano ya skuli ya Wesha hayafikii malengo ya utowaji wa elimu yenye bora kama inavyotakiwa.

 

Mh. Lela ambae pia ni muakilishi wa viti vya wasomi mkoa wa Kusini Pemba amesema hayo kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni tisa kwa ajili ya kulifanyia matengenezo banda la vyumba vitano vya kusomea la skuli ya Wesha vinavyotumiwa na wanafunzi wa sekondari na msingi.

 

Amesema wanafunzi wanachopaswa ni kujinza taaluma mbali mbali, lakini kutokana na ubovu wa madarasa ya skuli hiyo haitowi fursa mzuri ya  kujifunza kwani ni hatari kwao na hata kwa walimu kutoka na uchakavu wake

 

Akieleza changamoto hiyo mwalimu mkuu wa skuli ya msingi Wesha Mafunda Sudi Saburi amesema ubovu wa madarasa hayo inawakwaza katika utowaji wa huduma ya elimu kwani wakati wa mvua hushindwa kuyatumia.

 

Sheha wa shehia ya Wesha Haji Mohamed Ali amemshukuru waziri Lela na kuahidi kuutumia msaada bila ya ubadhilifu.

KUANGALIA VIDEO HII BOFYA HAPO CHINI.