Mikkel Damsgaard,
Liverpool , Leeds na Aston Vila huenda zikawasilisha ombi la muda wa lala salama ili kumsajili winga wa Denmark Mikkel Damsgaard , lakini Tottenham imejiondoa katika kivumbi cha kumwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 , ambaye nyota yake ilionekana wakati wa mashindano ya Euro 2020. (La Repubblica via Sport Witness)
Paris St-Germain bado hawajajibu ombi la Real Madrid kwa mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, na klabu hiyo ya La Liga imeweka tarehe ya mwisho ya Jumatatu kwa timu hiyo ya Ligue 1 kukubali au kukataa ombi hilo (Marca)
Sevilla haitakubali ofa ya chini ya euro 80m (pauni milioni 68.5) kwa beki wa Ufaransa Jules Kounde. Chelsea imekuwa ikihusishwa na uhamisho wa mchezaji huyo wa miaka 22 baada ya kumuuza mchezaji mwenzake wa kimataifa Kurt Zouma, 26, kwa West Ham. (Marca – in Spanish)
West Ham wanakaribia kumaliza makubaliano ya mkataba wa pauni milioni 25 kumsajili kiungo wa Croatia Nikola Vlasic, 23, kutoka CSKA Moscow. (Guardian)
Aston Villa wanaandaa ofa ya pauni milioni 15 kwa ajili ya kiungo wa kati wa miaka 21 wa Liverpool na England Curtis Jones, 20, ambaye bado hajaonekana katika kikosi cha Reds msimu huu. (Sun)
Everton, Brighton, Leeds na Crystal Palace wote wako kwenye mbio za kumsajili winga wa Manchester United na Wales Daniel James, 23, ambaye yuko huru kuondoka Old Trafford huku mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 36 Cristiano Ronaldo akiwa tayari kuwasili Juventus. (Star)
Everton wako kwenye mazungumzo juu ya makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon kutoka Dalian Professional ya China. Rafael Benitez, kocha wa Toffees alimsimamia kijana huyo wa miaka 31 nchini China na huko Newcastle. (Sky Sports)
Watford wanafanya mazungumzo na Birmingham juu ya kumuuza nahodha wa kilabu mwenye umri wa miaka 33 Troy Deeney kwa upande wa Mabingwa. (Athletic – subscription required)
Torino wanatafuta uhamisho wa mkopo kwa kiungo wa Leicester na Ubelgiji Dennis Praet, 27, ambaye hajajitokeza Foxes msimu huu. (Tuttomercatoweb, via Sport Witness)
Juventus watafuatilia uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji Axel Witsel, 32, na Massimiliano Allegri ikitaka kuimarisha safu yake ya kiungo wa kati. (Sky Sport – in Italian)
Klabu ya Serie A inaweza pia kumchukua mshambuliaji wa Paris St-Germain ya Argentina Mauro Icardi, 28, ambaye alifunga magoli 124 katika michezo 219 katika kipindi cha miaka sita kwa wapinzani wa Juve, Inter Milan. (Tuttosport – in Italian)
Bayern Munich wamefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa Austria Marcel Sabitzer, 27, kutoka kwa wapinzani wa Bundesliga RB Leipzig kwa euro 16m (£ 13.7m). (Bild – in German)
CHANZO CHA HABARI BBC