Thursday, January 16

Marafiki zangu walinitenga baada ya kugundulika kuwa naugua saratani

Maelezo ya picha,Hiral aliuzunishwa na marafiki zake wa karibu kwa kutokuwa karibu naye wakati anaugua saratani.

“Nilihisi vibaya kuona rafiki yangu wa karibu anachukua muda mrefu kuja kunitembelea hospitali,” Hiral Deugi anasema.

Ni binti wa miaka 24 sasa, ambaye aligundulika kuwa na saratani ya damu akiwa na miaka 20.

“Unapoanza kuumwa tu watu wanakukimbia, hawajui kuwa hiki ndicho kipindi muhimu unahitaji kusimuliana nao kuhusu mambo tuliyofanya zamani .

“Nimekuwa nikiwaona marafiki zangu kupitia kwenye mitandao ya kijamii wakienda kusheherekea , ni jambo zuri lakini lilikuwa likinifikirisha kuwa kwanini haji kunitembelea?’ Kilikuwa kipindi kigumu katika maisha yangu nilihitaji zaidi uwepo wake.”

Rafiki yake mmoja,Hiral alipomtembelea hospitali alisema kuwa hakufanya hivyo kabla kwani hakuwa na chochote cha kusema.

“Alivyoniambia hivi kwakweli nilijawa na hasira, niliona namna gani rafiki yangu kipenzi hanijali.”

‘Saratani yawabadilisha marafiki’

Masaibu aliyopitia Hiral sio ya kushangaza, Utafiti kutoka kwenye kituo cha Saratani umegundua kuwa 40% ndani ya asilimia 121 vijana wanaougua na saratani wamekuwa wakieleza kutengwa na marafiki zao pale tu walipokuwa wamegundulika na ugonjwa huo, robo tatu wamesema kuwa urafiki kati yao umebadilika.

23 year old Kathryn Rodwell who has Hodkin's lymphoma

CHANZO CHA PICHA,KATHRYN RODWELL

Maelezo ya picha,Marafiki wawili wa Kathryn’waliacha kuwasiliana naye wakati anapata matibabu ya saratani

Kathryn Rodwell, mwenye miaka 23 anatokea Kaskazini mwa Wales aligundulika na saratani akiwa mwaka wa pili chuoni. Anaendelea kupata matibabu ya kupandikiza seli.

Akiwa chuoni Kathryn alikuwa na marafiki watatu, lakini anasema kuwa mambo yalibadilika pale tu alipokuwa amegundulika kuumwa saratani.

“Nilijitahidi kuwasiliana nao, lakini sikufanikiwa . walinikatisha tamaa hata ya kuwasiliana nao.”

Anasema kuna rafiki mwengine alimpata alikuwa mchangamfu ila hakuvutiwa nae.

“Ukiwa na saratani unaweza kudhani hauna la kuzungumza zaidi ya ugonjwa tu, lakini unapokuwa na marafiki wa karibu mazungumzo yetu lazima yawe ya siku zote tuliyoyazoe.”

Kujihisi vibaya

Kati ya vijana 121 wanaosumbuliwa na saratani ,uchunguzi unasema kuwa bado ni jambo gumu sana kwa marafiki kubadilisha mazungumzo na rafiki anayesumbuliwa na ugonjwa huo.

photo of 22 year old Rian Harvey who was diagnosed with cancer as a teenager

CHANZO CHA PICHA,RIAN HARVEY

Maelezo ya picha,Rian anasema, saratani imenifundisha namna ya kuwatambua marafiki wa kweli ni wapi

Hili ndio jambo ambalo Rian Harvey aligundua pale tu alipokutwa na saratani ya leukaemia akiwa na miaka 14.

“Nilikuwa na marafiki ambao walioanza kunitenga na kuhakikisha kuwa hawatowasiliana na mimi.

“Hiki kipindi hiki nilumia sana, lakini kwasasa nimeanza kuelewa kitu gani kilichowafanya wasifike kunitembelea.

Akiwa na miaka 22 sasa,amepata kuwafahamu marafiki wa kweli kuwa ni wale ambao siku zote watakua na wewe kipindi chote cha matibabu.

“Kuna wengine wananiuliza kama ninahitaji kitu kutoka kwenye mgahawa wa McDonald,nilijihisi wa thamani tena.”

Je unawezaje kumuambia mtu mwenye saratani?

Helen Veitch kutoka Teenage Cancer Trust, kwasasa anaendesha kampeni ya namna marafiki wanavyotakiwa kuzidisha upendo kwa rafiki mwenye saratani.

“Ni jambo jema kuogopa pale unapokosa kitu cha kusema,”

“Lakini marafiki wengi wanapitia magumu mengi sana wakiwa mashulieni na ndio chanzo kinachowafanya wasiwe watu wa kuonyesha upendo .”

CHANZO CHA HABARI BBC