Mikono yetu ni muhimu katika kuongeza maana katika mazungumzo yetu. Mikono yetu inaweza kutusaidia kukumbuka maneno ya kusema na kusaidia katika kufikiri kwetu -inaweza hata kubadili sauti ambayo watu wanaisikia. Hata watu ambao wana ulemavu wa kuona tangu wamezaliwa wanaweza kuamini kuwa kuna ishara zinazofanana duniani kote ambazo wanaweza kuelewana kokote. Mwaka 2003 iliripotiwa kuwa wanajeshi wa Marekani walipofika Iraq walisalimiwa na raia wa nchi hiyo huku wakionyeshwa dole gumba juu. Kitendo kilichofanywa na raia hao huenda kikawa na tafsiri tofauti. Kwa mujibu wa taasisi inayojishugulisha na lugha nchini Marekani imeleeza kuwa mataifa mengi ya mashariki ya kati yamerithi tabia hiyo ya kidole juu baada ya ya vita ya ghuba ikiashiria kuwaunga mkono. Pengine walikuwa hawaoneshi kukerwa na ujio wao kama wengi walivyo fikiri. Safari nyingi za kidiplomasia kutoka kwa watu wa magharibi katika ukanda wa Mashariki ya kati zimeendelea kushamiri. Lakini hata watu wa magharibi nao wanautamaduni wa kuonesha kidole juu ila sio kote ulimwenguni itakua na maana sawa. Kwa watu wanaopenda kuelea angani, matumizi ya kidole gumba juu yanamaanisha “Naenda juu zaidi” Chanzo cha matumizi ya kidole gumba juu bado ni mtego uliokosa kuteguliwa, kuna watu wanadai kuwa ilianza kutumika baada ya vita vya ‘gladiator’, ambapo maamuzi ya kama wanaendelea na vita baada ya wanajeshi wao kufariki basi walichagua kidole gumba juu au auliwe. Pale adui anapoonesha kidole hiko ni alama kuwa amepona. Maeneo kama Marekani, Afrika, kusini mashariki mwa bara la Australia pamoja na nchi nyingine wao hutumia zaidi mdomo, kichwa , pua ila mdomo ndio maarufu zaidi. Kama ilivyo kwa raia wa Iraq kuwasalimia wanajeshi wa Marekani jambo hili linaweza kutafsiriwa tofauti kama salamu au kejeli, mataifa yaliyopo kwenye ukanda wa KImedeterani nchi kama Uturuki, Ugiriki na kusini mwa Italy kitendo hiki hakiruhusiwa unaweza ukakataa iwapo mtu akikuoneshea. Lugha nyingine ya ishara inayotolewa mfano ni katika kuonyesha kitu. Nick Enfield, Profesa wa lugha katika Chuo Kikuu cha Sydney anaeleza kuwa ishara ya kuonesha kitu imekuwa ikitumika toka enzi na mawasiliano yaliweza kufika lakini sio kila tamaduni kuonesha kwa kidole inaweza kukubalika. Sehemu kama Marekani,Afrika, kusini mashariki mwa Asia na Australia. Kutumia mdomo, pua kuwasiliana njia hizi zimezoeleka zaidi. Ni muhimu kutumia lugha hizi za ishara pale unapokuwa mawindoni kwa sababu utawasiliana na mtu mwingine bila kuwepo na taharuki yoyote. Swali ni kwamba, kama mawasiliano kwa ishara zinaweza kukubalika au kukataliwa kwa muktadha wa kiutamaduni, Je kuna ishara yoyote inayokubalika? “Watu kila mahali wanapenda mawasiliano ya aina hii, wanaweza kukuelekeza eneo leo wakitumia njia tofauti na watakavyofanya kesho,” Amesema Cooperridder. Mawasiliano kwa kutumia kiganja cha mkono yanaonekana kuwa maarufu zaidi ila bado hakuna aliyeweza kugundua chanzo chake. Leonardo da Vinci alishawahi andikia na kuchora pia katika karne ya 15. Lugha ya ishara huwa zinatengeneza maana moja kwa moja, kama vile “Sijui” au “kila kitu kipo sawa” hizi hutambulika kama nembo ishara. “Hizi hazitumiki kueleza kitu, hutumika kutoa maagizo kwa mtu kuwa aache anachokifanya au atoe majibu sahihi.” Licha ya utofauti , lakini kuna kuwepo na ujumbe ambao unawasilishwa ndani ya mawasiliano hayo ya ishara. Cornelia Müller, Profesa wa lugha toka Chuo Kikuu cha Viadrina Frankfurt, anaeleza kuwa zipo njia mbalimbali ndani ya lugha ya ishara. Amezifafanua aina nne za lugha ya ishara ya mkono: moja ikiwa kukunja kiganja cha mkono,kuchora, kuonyesha kwa vitendo na uwasilishaji. Aina ya kwanza inahusika zaidi matumizi ya mkono kufafanulia kitu. Mfano refa anapokuwa uwanjani hutumia zaidi mikono yake kuelezea mpira. Kuchora haijatofautiana na aina ya kwanza hii zaidi huelezea kitu husika. Aina ya tatu inatumika kueleza kitendo kinavyofanyika kama vile mtu anayejifanya anaandika ilihali sio kweli. Kikuu cha Jiji la Hong Kong, anafafanua kwamba aina za kimsingi zinapaswa kueleweka kwa wote. Watu wanaweza kusema wakati mtu anajaribu kuunda kitu mbele yao au wakati anaaga, hata ikiwa kile wanachojaribu kuwasiliana hakieleweki. Pamoja na nembo za ishara, ishara mpya zinaweza kuundwa. Harrison amesoma ishara katika mazingira ya viwandani, uzalishaji wa mmeaa viwandani unawafanya wafanyakazi wa viwanda hivyo kuzingatia uvaaji wa barakoa. Katika mazingira hayo, ishara ndio njia muhimu zaidi ya kuwasiliana. Harrison anasema kwamba watu huunda na kuelewa vitendo rahisi kama “kuacha”, “kurudia” na “zaidi”, na wanaweza kuweka alama kwa lugha yao ya ishara. Ambapo ishara inatumika zaidi ni pale mkono unapotumika kuonyesha umbo mfano kama kidole gumba. Hizi ni ishara holela za dhana ambazo zina wakilisha – hakuna kitu halisi juu ya kumwonyesha mtu kidole gumba ambacho kinamaanisha kuwa kila kitu kinaenda sawa. Kwa sababu ya utiifu wao, maana yao inaweza ikatafsirwa tofauti, anasema Gawne. Ishara ya kidole gumba juu imeonekana kutafsiriwa tofauti zaidi,wengi wakisema kuwa iinaweza kuwa ni ishara ya kihuni. Italia pamoja na mataifa mengi ya Ulaya ni jambo la kawaida kumuonyeshea mtu kidole cha kati ila taifa kama Croatia, inatumika katika kumuelezea mtu kuwa kitu alichokuwa anakitafuta hakipo. “Ningependa kusema kwamba njia zao za kujadili lugha ya ishara ni hafifu katika kutambua uhusiano wake na binadamu.” Mtandao imeleta njia nyingine kabisa za mawasiliano ambapo tunaweza kueleza jambo bila ya kutumia maandishi yasiyo rasmi – Lauren Gawne Ikiwa umeshindwa kuelezea jambo kwa maneno ya kawaida mara nyingi watu hutumia ili vikusaidie kueleza jambo ulilokusudia. Gawne anasema kuwa lugha ya maandishi huenda ikakosa kuelezea jambo fulani kwani maandishi yasiyo rasmi yanatumika kama suluhisho. Gawne amefanya kazi na Gretchen McCulloch na Jennifer Daniel kujumuisha utofauti mkubwa wa ishara za mikono katika kamusi rasmi ya Unicode ya lugha ishara. Kinachomfurahisha Gawne juu ya mawasiliano ya ishara za mikono katika kamusi ya Unicode ni kwamba ni ya kipekee sana. Ukweli kwamba (kama ishara halisi ya mikono) maana zao zinaweza kubadilika ni muhimu, anasema. Picha ya samaki nyota kila mtu anatambua kuwa ni samaki , lakini sura ya mkono inaweza kuwa na maana yoyote ambayo watumiaji wanataka kuielezea. Ishara za lugha vikatuni ya kwanza kutengenezwa ilikuwa ni ya mkono uliokunjwa, nyingine ikiwa vidole viwili vikiwa kwenye umbo la “V” pengine mwanzo zilitumika kama kuelezea mkasi lakini sasa ishara hii inaelezea amani. Gawne ana amini kuwa lugha ya ishara inaweza saidia kufikisha ujumbe kiurahisi zaidi ila kwa taifa kama India wenyewe wanaitafsiri kwa kuwaeleza watu njia ya kwenda msalani. Gawne ana amini kuwa lugha vikatuni inapotengenezwa basi itabidi iendelee kuwepo kwani kunaweza kuwa na mjumuisho wa lugha zitakazo saidia mawasiliano ndani yake. CHANZO CHA HABARI BBC
|
|
|