NA ABDI SULEIMAN.
TIMU ya wazee (veteran) kutoka kisiwa cha Pemba, imefanikiwa kutwaa ubingwa wa bonanza la mavetareni, lililofanyika katika uwanja wa michezo Gombani kwa mikwaju ya penant 4-2.
Bonanza hilo lililoandaliwa na Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, nakuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali na mashabiki wa soka Pemba.
Timu hizo zilikianza kipindi cha kwanza kwa kasi kubwa, huku kila timu ikihitaji ushindi uwanjani hapo, huku wakichezeshwa na waamuzi kutoka Academy ya JKU.
Hata hivyo licha ya kila timu kufanya mabadiliko ya wachezaji wao uwanjani hapo, lakini jitihada zao ziligonga mwana na kupelekea mchezo huo kumalizika timu zikiwa bila ya kufungana uwanjani hapo.
Kwa upande timu ya Unguja iliongozwa na maveterani Saleh Ahmed Machupa, Omar Yussuf Cheupe, Aliy Sharif Adofu, Innocent Haule na Ramadhan Hamza Kidulu.
Kwa upande wa Mavetereani wa Pemba iliongozwa na Suwedi Hamad, Rajab Hamad, Mussa Bajaka, Khamis Wawingwi, Omar Mjaka na Mkubwa Khamis.
Akizungumza na wanamichezo Mbali Mbali Unguja na Pemba, mara baada ya kumilika kwa mashindano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, aliipongeza Wizara ya Habari Zanzibar kwa mikakati yake ya kuhakikisha wanainua soka la Zanzibar.
Alisema kufanyika kwa bonanza hilo na kuwashirikisha wachezaji wa zamani wa Mpira wa Miguu, ni kuonyesha jinsi gani serikali kupitia wizara inathamini juhudi na mchango wa wachezaji hao.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatama Hamad Rajab, aliwataka maveterani hao kusaidia serikali katika jitihada zake za kukusaza soko la Zanzibar.
Bingwa katika bonanza hilo alipatiwa kikombe, medali na fedha taslimu shilingi Milioni 1.5, huku mshindi wa pili akipatiwa kikombe, medali na shilingi Milioni Moja