Wakati Ole Gunnar Solskjaer anazungumza na waandishi wa habari kwa njia ya Zoom siku ya Ijumaa mchana, tayari meneja huyo wa Manchester United alikuwa anajua wazi kwamba Cristiano Ronaldo atarejea Old Trafford.
Licha ya kuzagaa kwa tetesi nyingi kwamba Ronaldo anajiandaa kutua Manchester City, mpaka usiku wa alhamis maafisa wa klabu hiyo walikuwa na uhakika kuwa mshindi huyo wa tuzo 5 za mwanasoka bora wa dunia Ballon D’Or anarejea ligi kuu England akiikacha Etihad Stadium na kuelekea Old Trafford, umbali wa maili nne tu.
Msukumo wa kumnasa Ronaldo, ulifanyika asubuhi ya Ijumaa,pale kocha wa zamani wa United Sir Alex Ferguson alipohusishwa.
Ukaribu wa Ferguson na Ronaldo ni mkubwa. Kwa muda mrefu Ronaldo bado anamchukulia Mscotland huyo kama ‘The Boss’ hata baada ya kujiunga na Real Madrid mwaka 2009. Ferguson alimtaka Ronaldo kurudi Old Trafford, akijua kwamba atakuwa shujaa. Angefanya tofauti, angepoteza sifa yake, wakati huu United ikihaha kurejea kwenye makali tangu kustaafu kwa Ferguson mwaka 2013.
Maneno ya Ferguson yalifuatia ujumbe wa ushawishi wa wachezaji wenzake na Ronaldo wa zamani Rio Ferdinand na Patrice Evra. Mchezaji mwingine wa zamani ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa ufundi wa United Darren Fletcher alielezwa kwmaba na yeye alikuwa sehemu ya kushawishi pamoja na mchezaji mwenzake kenye timu ya taifa ya Ureno Bruno Fernandes.
Wakati Solskjaer anazungumza na vyombo vya habari, kocha wa Juventus Max Allegri alikuwa tayari ameiambia dunia kwamba Ronaldo anaondoka kalbuni hapo. Uhamisho huo ulikuwa tayari umekamilika.
Kama ilivyo kawaida yake, Solskjaer hakutaka kusema lolote mapak kila kitu kiwe kimekamilia. Karibu mara tatu alikwepa kutoa majibu kuhusu Ronaldo, kabla ya mwanidhi wa Telegraph kupata nafasi hiyo.
Aliuliza kama mmoja wa wachezaji bora duniani anapatikana, Je Manchester United inawez akujaribu kumsajili?
“Sikutarajia kwamba Cristiano angeondoka Juventus,” alisema Solskjaer. “kumekuwa na tetesi.
“Tumekuwa na mawasiliano mazuri. Najua Bruno amekuwa akizungumza naye pia. Anajua hisia zetu kuhusu Ronaldo. Kama anaondoka Juventus, anajua fika tupo kwa ajili yake.”
Mpaka wakati huo, ofa rasmi ya €23m ilikuwa ishawasilishwa tayari Juventus. Baada ya masaa matatu baadae, United walithibitisha kuwa makubaliano ya kumrejesha Ronaldo yalikuwa yamefikiwa.
United ilitokea kusikojuliakana
Gareth Bale na Ronaldo walikuwa wanasakwa na United ili kusaidia timu hiyo baada ya kuondokewa na Ferguson mwaka 2013.
Tetesi za kurejea Old Trafford zimekuwa za muda mrefu, ingawa haikuwa inaonekana kama jambo lisilowezekana kirahisi kumnasa nyota hyo aliyefunga mabao 118 katika michezo 292 aliyoichezea United kati ya mwaka 2003 mpaka 2009 na kuisaidia timu hiyo kutwaa makombe matatu ya ligi kuu England, na moja la ligi ya mabingwa Ulaya.
United iliendelea kufuatilia hali ya mambo Juventus karibu msimu mzima wa usajili, Juve ikipitia wakati mgumu wa kifedha ikikabiliana na UEFA kuhusu mpango wake wa kuanzisha ligi ya European Super League pamoja na vilavu vingine vitano vya Uingereza.
Milango ya mawasiliano yalikuwapo baina ya United na wakala wa muda mrefu wa mchezaji huyo, Jorge Mendes. Tetesi zilipoaza kwamba Ronaldo anataka kujiunga na Paris St-Germain kama alivyosema Solskjaer, United ilikuwa nyuma ya pazia. Walihisi kwamba Ronaldo angetamani kubaki Turin kumalizia mwaka mmoja uliosalia kwenye mkataba wake.
Lakini baada ya kusikia Manchester City wanahusishwa na Ronaldo, hapo ndipo masikio yao yaliposimama.
Mpaka alhamisi usiku, City walikuwa ama wanafikiria mpango huo wa Ronaldo ama kama inavyoelezwa walikuwa wamemalizana nae. Vyanzo vyingi vinasema walikuwa na nia lakini bado hakukuwa na makubaliano yaliyokamilika
Ikawa United pekee waliojitokeza na kutupa ndoano yao.
Kwa nini sasa?
Ronaldo alisajiliwa Manchester United mwaka 2003 na kuifungia klabu hiyo mabao 118
Kwa United, kurejea kwa Ronaldo kunauhusiano na nyakati za mafanikio za Klabu hiyo.
Katika miaka mitatu kati ya msimu wa 2006-07 na 2008-09, mreno huyo alionyesha kiwango cha hali ya juu. Pamoja na hilo, usajili wake wa sasa unahusu sasa na kiwango chake cha sasa.
Kupatiwa mkataba wa miaka miwli United ni ushahidi tosha kuhusu uwezo wa Ronaldo ana atathibitshwa kabla ya Jumanne dirisha la usajili litakapofungwa rasmi.
United inadhani Ronaldo anaweza kuendana na mipango yao ya kuunganisha wachezaji wakubwa wa kiwango cha juu na vijana wenye vipaji. Wanadhani kwamba kikosi chao ni moja kati ya kikosi chenye vijana wengi kwenye ligi kuu England.
Kwa kuongezea, wanaona usajili wa Rafael Varane na Jadon Sancho – ni ushahidi kwamba United bado inaweza kuwavutia wachezaji wakubwa.
Huku kukiwa na suala linaloendela sasa kuhusu kuruhusiwa ama kutoruhusiwa kwa wachezaji kucheza mechi za kufuzu kombe la dunia mwezi ujao, mshambuliaji wa United Edinson Cavani ameonekana kuhoji uamuzi wa bodi ya Ligi kuu England ya kuwanyima fursa wachezaji kuziwakilisha nchi zao, kama watalazimika kukaa karantini kwa siku 10 watakaporejea England.
United washaweka bayana kwamba hawana mpango wa kumuuza Cavani, 34 au kuvunja mkataba wake alioshawishiwa na Solskjaer kuusaini mwezi Mei.
Hoja hapa haitakuwa namba gani ya jezi atavaa Ronaldo hata kama Cavani wataamua kumuachi jezi yake namba 7, lakini kanuni za ligi kuu zinakataza kubadilishaa jezi katikati ya msimu, mpaka kuwe na mazingira ya kipekee sana – Lakini ikifanyika hivyo huenda ikatingisha uhusiano wake na mchezaji huyo anayetumikia adhabu yake aliyopewa na Chama cha soka England ya kutocheza michezo mitatu kutokana na kuchapisha ujumbe usiofaa kwenye mtandaowa kijamii.
Mipango ya kumkaribisha nyumbani Ronaldo
Inatarajiwa atafanyiwa vipimo vya afya nchini Ureno kabla ya kuungana na wachezjai wenake wa timu ya taifa ya Ureno kwa ajili ya mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Azerbaijan inayopigwa Jumanne Septemba 7.
Huenda akanza kucheza dhidi ya Newcastle, Jumamosi inayofuata. Mara ya mwisho Ronaldo alicheza dhidi ya Newcastle akiwa Manchester United kwenye dimba la Old Trafford, alifunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 6-0. Ndo maana ujio wake wa kurejea Old Trafford umepokelwa vyema na mashabiki wa klabu hiyo.
Mafanikio ya kweli ya nyota huyo mwenye miaka 36 yatapimwa kwa kile kitakachotokea uwanjani – lakini kama watatumia kile alichofanya siku hiyo, kununuliwa kwa Cristiano Ronaldo Manchester United kwa uhakika ni mshindi wa kweli.
CHANZO CHA HABARI BBC