Thursday, January 16

HABARI PICHA: Ujenzi wa barabara kongwe Wete-chake waanza kwa kikao.

WATENDAJI kutoka Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, wakifuatilia kwa makini kikao cha pamoja baina ya Wakuu wa Mikoa miwili ya Pemba na Wakuu wa Wilaya na watendaji kutoka kampuni ya MECCO yenye dhamana juu ya ujenzi wa Barabara ya Wete-Chake Chake, kikao kilichofanyika Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, akizungumza katika kikao cha pamoja baina ya wakuu wa Mikoa, Wilaya ya na Watendaji kutoka kampuni ya MECCO juu ya uwanzaji wa Ujenzi wa barabara ya Wete-Chake Chake, halfa iliyofanyika Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba

 

MKURUGENZI Mwendeshaji kutoka Kampuni ya MECCO Abdulikadir Mohammed, akizungumza katika kikao cha pamoja baina ya Wakuu wa Mikoa, Wilaya na viongozi kutoka Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, kikao kilichofanyika Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Amour Hamil Bakari, akizungumza na kuwakaribisha wageni katika kikao cha pamoja, baina ya watendaji wa Wizara hiyo, wakuu wa Mkoa na Wilaya za Pemba na watendaji kutoka Kampuni ya MECCO juu ya ujenzi wa barabara ya Wete-Chake Chake.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)