Wakati muendelezo wa utekelezaji mradi wa VIUNGO Zanzibar umeingia mwaka wa wapili kamati ya ushari ya mradi huo inakutana katika ofisi mradi huo zilizopo mwanakwerekwe mjini Unguja.
Kamati hio ya ushauri yenye wajumbe 20 ambao ni wakurugenzi kutoka taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi zinazojihusisha iwe kwa namna moja au nyengine na utekelezwaji wa mradi huo.
Kamati hio ambayo hukutana mara nne kwa mwaka ambapo kwa mwaka wakwanza wamekutana chini ya mwenyekiti wa mpito Foum Ali Garu na kufanya vikao vyake vyote vilivotakiwa kwa mujibu wa andiko la mradi huo.
Lengo kuu la kamati hio ni kutoa ushauri kuhakikisha utekelezaji huo wa mradi unatekelezwa vizuri na kunufaisha walengwa wote hatimae mabadiliko yaweze kuonekana kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Wakati hayo yakijri katika mkutano huu wa leo wajumbe hao wamepata Mwenyekiti mpya wa kamati hio ya ushauri ,Mohamed Khamis Rashid ambae ni Mkurugenzi wa Idara ya kilimo Zanzibar.
Awali mara ya kukabidhiwa nafasi hio Mwenyekiti huyo aliwataka wajumbe hao kuhakikisha wanauelewa vyema mradi huo ili waweze kutoa ushauri wenye tija kwa maslahi ya Taifa.
Akifungua mkutano huo Meneja mkuu wa mradi huo Amina Ussi Khamis alisema wajumbe wa mkutano huo wanapaswa kuwa huru na kutoa maoni yao kwani maoni hayo ndio yatakayoongeza ufanisi ikiwemo kukuza na kuendeleza mradi huo.
Mradi huo wa viungo unatekelezwa na Taaissi ya PDF,kwa kushirikiana na TAMWA-ZNZ pamoja na CFP Chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya kwa muda wa miaka mine huku lengo kuu likiwa ni kuwainua wakulima wa Zanzibar kiuchumi kutoka shehia mbali mbali za Unguja na Pemba.