Thursday, January 16

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 13.09.2021: Phillips, Olmo, Fofana, Rodriguez, Isak, Dembele, Vlahovic

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anaitaka klabu hiyo kumsaini kiungo wa kati wa Leeds na England Kalvin Phillips, 25, msimu ujao . (Fichajes, in Spanish)

Barcelona inamlenga mchezaji wa RB Leipzig Dani Olmo , huku Manchester United , Juventus na Bayern Munich zikionesha hamu ya kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 23.. (Marca, in Spanish)

 

Beki wa Leicester City na Ufaransa Wesley Fofana, 20, anasema kwamba Real Madrid ndio klabu kubwa duniani na kwamba ni ndoto yake kuichezea klabu hiyo.. (YouTube, via Marca)

Omar Fofana

Everton ilishindwa kumuuza kiungo mchezeshaji wa Colombia James Rodrigues kutokana na mshahara wa £250-000- kwa wiki . (Football Insider)

Baadhi ya klabu za Uingereza zinamnyatia mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 21 , licha ya mchezaji huyo kutia saini kandarasi ya muda mrefu na Real Sociedad. Arsenal na Chelsea awali zimeonesha hamu ya kumsajili mchezaji huyo. (Fichajes via Teamtalk)

Tottenham Hotspur imefungua mazungumzo na Ajax kuhusu uwezekano ya kumsajili beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 20 Jurrien Timber.. (Todofichajes in Spanish)

Ousmane Dembele

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Barcelona inapanga kufanya mazungumzo na ajenti wa Ousmane Dembele kuhusu kuongeza kandarasi ya mshambuliji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24, lakini hakuna mkutano uliofanyika kufikia sasa.. (Mundo Deportivo, in Spanish)

Mchezaji wa AC Milan Franck Kessie, 24, anavutia hamu kutoa klabu ya Barcelona – lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Liverpool, Tottenham na PSG ili kumsajili kiungo huyo wa Ivory . (Mundo Deportivo, in Spanish)

Mshambuliaji wa Serbia 21, Dusan Vlahovic, ambaye alivutia hamu kutoka klabu za Tottenham na Atletico Madrid mwisho wa msimu uliopita , yupo katika mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba wake na klabu ya Florentina. (Fabrizio Romano)

Houssem Aouar
Maelezo ya picha,Houssem Aouar

Kiungo mchezeshaji wa Ufaransa Houssem Aouar, 23, amepinga mazungumzo yanayomuhusisha yeye na klabu ya Arsenal na anasema anataka kuisadia Lyon kufuzu katika kombe la klabu bingwa Ulaya.. (Metro)

CHANZO CHA HABARI BBC