Thursday, February 27

Mkoa wa Mjini Magharibi waibuka na ushindi wa jumla elimu bila ya malipo.

 

NA ABDI SULEIMAN.

MASHINDANO ya Elimu bila Malipo 2021 yamefikia tamati katika Kisiwa cha Pemba, kwa Mkoa wa Mjini Magharibi kuibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo.

Mkoa huo umeweza kuibuka mshindi baada ya kupata vikombe vingi kuliko mikoa mengine, katika mashindano hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Michezo Gombani.

Katika maadhimisho hayo washindi wa mashindano hayo waliweza kukabidhiwa vikombe vyao na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Massoud Othman, kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.

Huku Mkoa wa Kaskazini Pemba na Mkoa wa Kaskazini Unguje zimefanikiwa kuibuka kuwa mikoa yenye nidhamu katika mashindano hayo.

Kwa upande wa Mashindano ya Riley 100 x 400, wanaume Sekondari skuli ya Ndijani imeibuka mshindi wa kwanza, nafasi ya pili ikaenda kwa skuli ya Nyerere na Gando Sekondari ikashika nafasi ya tatu.

Kwenye mita 200 wanawake skuli za Msingi Khadija Mtumwa Mabrouk (kigunda), nafasi ya pili ikaenda kwa Zayna Mohamed Idrissa (Sebleni) na Maryam Mussa Ame (Gando).

Hata hivyo katika mashindano hayo michezo mbali mbali imefanyika ikiwemo Resi za Magunia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, upasuaji wa mabofu kwa wanafunzi wa Maandalizi, mbio za mbatata kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, pamoja na riadha mita 50 kwa wanafunzi wa maandalizi.