Akinamama wenye VVU wapumzike baada ya kujifungua-Dk. Rahila
NA ZUHURA JUMA, PEMBA
AKINAMAMA wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wametakiwa kupata mapumziko baada ya kujifungua, ili wapate kuimarika kiafya pamoja na mtoto wake, huku akifuata maelekezo ya daktari wakati gani kwake anaweza kubeba mimba.
Aizungumza na mwandishi wa habari hizi, Msimamizi wa Vituo vya kutoa huduma kwa watu wenye VVU Dk, Rahila Salim Omar alisema, mwili unapotoa kiumbe unahitaji kujirejesha tena katika hali ya kawaida na ndipo uweze kubeba mimba nyengine.
Alisema kuwa, wakati wa ujauzito kinga ya mwili inashuka, kwa hiyo uwezekano wa kupata maambukizi mengine unakuwa ni mkubwa kiasi kwamba anaweza kupata maambukizi mengine yatakayoweza kumsababishia mtoto kupata VVU.
Alifahamisha kuwa, afya ya mama huyo inakuwa bado haijarudi katika hali yake ya kawaida, hivyo ...