Thursday, February 27

afya

Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ZAC wameandaa majadaliano ya elimu ya Ukimwi.
afya, ELIMU

Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ZAC wameandaa majadaliano ya elimu ya Ukimwi.

  Tukiwa tumo katika maadhimisho ya siku 16 za uanaharakati za kupinga ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto Leo Afisa Mdhamini Afisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Ahmed Abubakar Ali alikuwa Mgeni rasmi katika majadiliano ya Elimu ya UKIMWI kwa vijana. Akizungumza na vijana Ahmed amewataka vijana kujitambua na kuthamini utu wao huku wakiwa na uthubutu wa kukataa kurubuniwa na kutumiliwa vibaya katika jamii. Akizungumzia suala la udhalilishaji mdhamini huyo amesema tukiwa tumo katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga udhalilishaji na ukatili wa wanawake na watoto vijana wanapaswa kuwa tayari kubeba agenda ya kuwekeza katika kuzuwia unyanyasaji na ukatili wa wanawake na watoto huku wakiwa mstari wa mbele kujiepusha kudhalilishana wao kwa wao au kuwadhalilisha wen...
TRA yakabidhi bati uongozi wa skuli ya Michenzani Mkoani
afya, Biashara

TRA yakabidhi bati uongozi wa skuli ya Michenzani Mkoani

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA MWENYEKITI wa Kamati ya Ujenzi ya Skuli ya Michenzani Hamud Malim Khami, ameushukuru uongozi wa TRA Mkoa wa kikodi Pemba, kwa kuwakabidhi bati 50 zenye thamani ya shilingi Milioni 1,740,000/ ikiwa ni utekelezaji wa ahadi kwa skuli hiyo. Alisema kwa sasa wanahitaji bati zisizopungua 300, kwa ajili ya uwezekaji wa bweni la wanafunzi wakike, wakati watakapokua wanakabiliwa na mitihani yao ya taifa. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa bati hizo, kutoka kwa watendaji wa TRA Mkoa wa kikodi Pemba, huko Chokocho Wilaya ya Mkoani, ikiwa ni Wiki ya Shukurani kwa mlipakodi Pemba, ilioambatana na kauli mbiu “Kodi Yetu, Maendeleo Yetu, Tuwajibike” yalyoandaliwa na TRA Pemba.   Alisema kwa sasa bweni hilo linakabiliwa na changam...
BIMA ya Jubilee life inathamini mchango wa walimu
afya, ELIMU

BIMA ya Jubilee life inathamini mchango wa walimu

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA MENEJA wa Bima ya Jubilee Life Bertha Magoli, amesema bima hiyo inathamini mchango wa walimu katika suala zima la bima ya maisha, kutokana na umuhimu wa kazi yao ya kufundisha. Alisema walimu wamekua wakikumbana na changamoto nyingi katika muda wao wote wanapokua skuli, hivyo bima ya Maisha imekuja kumfuta machungu mwalimu pale anapopatwa na tatizo. Hayo aliyaeleza wakati wa utambulisho wa mdhamini na utoaji wa mada ya kwanza Bima ya Maisha kwa vikundi, wakati mkutano wautoaji wa elimu ya Bima kwa SACCOS ya Walimu Pemba, mkutano uliofanyika Tibirinzi nje kidogo ya Mji wa Chake Chake. Ailisema bima ya maisha imegawika sehemu mbili, sehemu moja ni bima ya mtu mmoja mmoja, ambapo mwanachama anachukua ulinzi wake mwenyewe. Bima ya pili ni kikundi, ...
Wananchi watakiwa kuchukua thadhari kwa kusafisha maeneo ya makaazi
afya

Wananchi watakiwa kuchukua thadhari kwa kusafisha maeneo ya makaazi

NA ABDI SULEIMAN,PEMBA WANANCHI Kisiwani Pemba wameshauriwa kuendelea kuchukua tahadhari juu ya maradhi ya mripuko, katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Ushauri huo umetolewa na viongozi wa Serikali Pemba, wakati walipokua wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tafuti, juu ya hali ya mvua zinazoendelea na suala la maradhi ya mripuko. Viongozi hao wamesema ili kusitokea maradhi hayo, wananchi wanapaswa kusafisha maeneo yao yaliowazunguruka, kuacha kutupa takataka ovyo katika vyanzo vya maji, pamoja na kusafisha mitaro ya maji taka ili isiweke uchafu. Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, alisema mpaka sasa ndani ya Mkoa huo, hakuna kesi ya kipindupindu iliyoripotiwa au kutoka kwa maradhi yoyote katika kipindi hiki cha mvua. ...