Serikali itaendelea kujenga hospitali, kuimarisha huduma za afya
NA ZUHURA JUMA, PEMBA
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kujenga hospitali na vituo vya afya vyenye vifaa vya kisasa ili kuwapatia huduma bora za afya wananchi wake.
Akizungumza wakati akifungua hospitali ya Wilaya iliyopo Kinyasini Wilaya ya Wete, Dk. Mwinyi alisema tayari zimeshajengwa hospitali za Wilaya kwa unguja na Pemba huku Serikali ikiendelea kujenga hospitali za mikoa, rufaa na mwanzo (dispensaries na vituo vya afya) ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya bila ya usumbufu.
Alisema kuwa, ujenzi wa hospitali hizo na vituo vya afya vitawapunguzia wananchi kwenda masafa marefu kuifuata huduma hiyo, sambamba ya kupata huduma bora kutokana na vifaa vya kisasa vilivy...