Monday, November 25

afya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Awatembelea na Kuwafariji Wagonjwa Katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.
afya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Awatembelea na Kuwafariji Wagonjwa Katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.Dr.Msafiri Marijani, alipowasili katika viwanja vya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kuwatembelea na kuwajulia hali Wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimjulia hali mmoja wa Wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Ndg. Said Mussa, aliyelazwa katika Wodi ya Wagonjwa waliopata ajali RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimjulia hali Mtoto Samir Haji akiwa amepakatwa na Mama yake Bi. Zulfa Vuai Mwinyi, alipotembelea Wodi ya Watoto katika jengo la Taasisi ya ‘ Neurosurgical Institute’ katika Hopitali ya...
VIDEO: Bidhaa zenye thamani ya zaidi ya shilingi 30,000,000 zimeangamizwa .
afya, Kitaifa, Sheria

VIDEO: Bidhaa zenye thamani ya zaidi ya shilingi 30,000,000 zimeangamizwa .

  NA KHADIJA KOMBO –PEMBA. Bidhaa mchanganyiko zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni thelathini (30,000,000) zilizoharibika zimeangamizwa kutokana na kuwa hazifai kwa matumizi ya binaadamu. Akizungumzana katika kazi ya uangamizaji huko Pujini Mkurugenzi wa Idara ya kumlinda mlaji na udhibiti wa bidhaa bandia  Zanzibar Alya Emannuel Juma amesema bidhaa hizo zimekamatwa kutoka kwa wafanya biashara mbali mbali kutokana na ukaguzi wanaoufanya katika maduka na maghala ya wafanyabiashara hao. Amesema baadhi ya bidhaa bado hazijapitiwa na wakati lakini kutokana na utunzaji mbaya wa bidhaa inasababisha kuharibika hivyo amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wana panga bidhaa zao vizuri ili zisiweze kuharibika. Naye Ali Omar Masoud afisa kutoka Tume ya ushindani halali w...
Jinsi msongo wa mawazo unavyosababisha mvi na jinsi ya kuzuia hali hiyo.
afya, Kitaifa

Jinsi msongo wa mawazo unavyosababisha mvi na jinsi ya kuzuia hali hiyo.

Kadri umri wa mwanadamu unavyosonga kuongezeka, ni kawaida kwa nywele kubadili rangi na kuwa za kijivu au nyeupe. Watu wengi hugundua kwamba mvi huanza kuota mapema miongoni mwa watu wanaofanya kazi zilizo na shinikizo sana kama vile miongoni mwa marais, maafisa wakuu watendaji na hata maafisa wakuu wa fedha. Mpaka sasa hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kwamba msongo wa mawazo humfanya mtu kuota kwa mvi mapema. Lakini wataalamu wanasema hali ya kuota mvi mapema kunaweza kudhibitiwa. Kulingana na utafiti mpya wa Chuo Kikuu cha Columbia uliochapishwa katika jarida la eLife: wakati chanzo cha mafadhaiko kinapoondolewa, nywele zinaweza kurudi kwenye rangi yake ya kawaida. Kwanini Ghana haina 'wanawake wazee'? Kwa miongo kadhaa tum...
VIONGOZI wa Serikali Kisiwani Pemba waunda mikakati juu ya kujilinda na kujikinga na wimbo la tatu la Corovid 19.
afya

VIONGOZI wa Serikali Kisiwani Pemba waunda mikakati juu ya kujilinda na kujikinga na wimbo la tatu la Corovid 19.

  NA ABDI SULEIMAN. VIONGOZI wa Serikali Kisiwani Pemba, wamesema kuwa licha ya kisiwa hicho kuwa na bandari bubu nyingi, hivyo watahakikisha mkazo zaidi unawekwa katika maeneo hayo ili kudhibiti wimbi la tatu la Covid 19 kutokea. Kisiwa cha Pemba kimejaaliwa kuwa na bandari bubu zaidi ya 300, hivyo mikakati hiyo ni pamoja na elimu kutolewa, kupimwa kwa afya wanaoingia nchini, pamoja na kuwekwa vifaa mbali mbali vya kukabiliana na wimbo hilo. Viongozi hao waliyaeleza hayo katika kikao cha kuunda mkakati juu ya kujilinda na kujikinga na wimbo la tatu la Corovid 19, ambalo tayari limeashaanza kwa kasi na dalili zake kubadilika. Akichangia katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Wete Mgeni Khatib Yahya, alisema mikakati zaidi inahitajika katika bandari bubu kuzuilika kut...
FAMILIA ya Amed Alfalas, kutoka Dubai na wasaidizi wake wamewasili Kisiwani Pemba.
afya, Kitaifa

FAMILIA ya Amed Alfalas, kutoka Dubai na wasaidizi wake wamewasili Kisiwani Pemba.

Na Shaib Kifaya  Pemba. FAMILIA ya Amed Alfalas, kutoka Dubai akiongoza na wasaidizi wake  Umewasili Kisiwani Pemba na kutembelea hospital  tofauti  kwa lengo la kuangalia Changamoto  na kuzisaidia. Hayo yamelezwa na Waziri wa afya Ustawi Wajamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar, Nasoor Ahmed Mazrou,  wakati wa Ziara hiyo huko hospital ya Vitongoji Cottage. Alisema lengo la Mfadhili huyo Armed Alfalas Kutoka Dubai ni  kusaidia Vifaa tiba na mashine mbali mbali  kwa hospital  kwa vile ameona kuna mapungufu makubwa yanayohitajika wakati wa utoaji wa huduma kwa wananchi na kuahidi kujenga kituo cha Usafishaji damu cha Wagonjwa wenye matatizo ya Figo ili kuepuka gharama za kwenda Unguja kimatibabu pamoja na kuahidi kujenga jengo la mama na mtoto na kutoa mashine mbali mbali  za uchunguzi...