Monday, November 25

afya

Tanzania yathibitisha wimbi la tatu la Corona
afya

Tanzania yathibitisha wimbi la tatu la Corona

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amethibitisha kwamba kuna viashiria vya wimbi la tatu la virusi vya Corona nchini humo. Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika mkutano wake na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania(TEC), Rais Samia amesema zipo ishara ndani ya nchi hiyo kwamba janga hilo lipo. ‘Kama tunavyojua duniani sasa hivi kuna wimbi la 3 la Corona, tumetoka kwenye wimbi la kwanza Tanzania tumeingia tumeingia, limekwenda limekwenda limepungua kidogo tumeingia wimbi la pili, tumekwenda na sasa wimbi la tatu’. Rais Samia alisema ‘Ishara ndani ya nchi tayari zinaonekana, tayari tuna wagonjwa ambao wemeshaonekana kwenye wimbi hili la tatu’, alisema Rais Samia akirejea pia kukumbusha ziara yake katika Hospitali ya Mwananyamala jiji...
Madaktari Watakiwa Kutowa Elimu Kwa Jamii Ili Kuepesha Maradhi Yasioambukiza.
afya

Madaktari Watakiwa Kutowa Elimu Kwa Jamii Ili Kuepesha Maradhi Yasioambukiza.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho Tanzania  Kazim Akbar Dhalla akitoa mafunzo kwa madaktari wa Zanzibar kuhusu upofu wa macho unaosababishwa na maradhi yasioambukizwa huko Hospitali kuu ya Mnazimmoja, mafunzo hayo yatatolewa kwa  muda wa siku tatu kuanzia tarehe 23 hadi 25 mwezi huu.  Dkt Salama Asaa Ali akichangia mada baada ya kupata mafunzo kuhusu upofu wa macho unaosababishwa na maradhi yasiyoambukizwa kutoka kwa Bingwa wa Magonjwa ya Macho Tanzania  Kazim Akbar Dhalla huko Hospitali kuu y a Mnazimmoja mafunzo hayo yatatolewa kwa  muda wa siku tatu kuanzia tarehe 23 hadi 25 mwezi huu.  Picha na Bahati Habibu -- Maelezo. Na Khadija Khamis – Maelezo  Daktari Bingwa wa Macho Tanzania  Dk.Kazim Akber Dhalla amewataka madaktari kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuepukana na...
VIDEO: SOS yakabidhi bima za afya kwa watoto wenye mahitaji maalum Dodo Pujini..
afya, Wanawake & Watoto

VIDEO: SOS yakabidhi bima za afya kwa watoto wenye mahitaji maalum Dodo Pujini..

NA KHADIJA KOMBO- PEMBA. Wazazi pamoja na walezi wametakiwa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya Afya mapema pindi wanapopatwa na tatizo la kiafya na kupatiwa matibabu kwa haraka ili kukinga athari zinazoweza kujitokeza . Wito huo umetolewa na Daktari  dhamana Wilaya ya Chake Chake ( DMO ) Mohammed Ali Jape wakati alipokuwa akikabidhi kadi za bima za Afya kwa watoto wenye mahitaji maalum zilizotolewa na shirika la SOS huko Dodo Pujini katika Wilaya ya Mkoani. Amesema Bima ya afya ni muhimu kwani inasaidia kupata huduma hizo kwa urahisi hivyo amewataka wazazi kuzitunza vizuri na kuzitumia kila wanapokwenda katika vituo vya afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Kwa Upande wake Mratib wa Shirika la SOS Kisiwani Pemba  Gharib Abdalla Hamad  amesema lengo la SOS kukabidhi bim...
Wananchi Watakiwa Kuchukua Tahadhari Juu ya Wimbi Jipya la Virusi vya Maradhi ya Corona Linalizuka Duniani.
afya

Wananchi Watakiwa Kuchukua Tahadhari Juu ya Wimbi Jipya la Virusi vya Maradhi ya Corona Linalizuka Duniani.

Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza  Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Mhe.Nassor Ahmed Mazrui  wakati akitoa taarifa kuhusu wimbi la tatu la maradhi ya korona katika ukumbi wa wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar . Muandishi Muandamizi  wa Bomba FM. Mwinyi Sadala akitaka kufahamu kuhusu maradhi ya korona kwa upande wa Zanzibar  kwa Mhe Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar. Na Rahma Khamis Maelezo  Zanzibar.   Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto  Zanzibar imewataka wananchi kuchukua tahadhari zaidi juu ya wimbi jipya la  viashiria vya maradhi ya Corona lilizozuka Duniani. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kuzuka kwa wimbi hilo Waz...
Zanzibar Inaunga Mkono Azma ya Bohari ya Dawa (MSD) Kujenga Kiwanda cha Dawa Zanzibar.
afya

Zanzibar Inaunga Mkono Azma ya Bohari ya Dawa (MSD) Kujenga Kiwanda cha Dawa Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Mej. General Saali Mhidze, alipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Mej.General Saali Mhidze alipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaunga mkono azma ya Bohari ya Dawa (MSD) ya kutaka kujenga kiwanda cha dawa hapa Zanzibar. Rais Dk. Mwinyi alitoa pongezi hizo leo Ikulu Jijini Zanz...