MAKALA VIDEO: SAUTI YAO. JEE! unataka kujua katika Sauti yao leo kutasikika sauti ya nani?
NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Wahenga wanasema Chanda chema huvikwa pete ikiwa na maana ya kwamba unapofanya jambo jema basi daima na wewe utalipwa mema na wengine wakadiriki kusema kwamba mcheza kwao hutunzwa yote hayo ni katika kusisitiza kufanya kila lililo jema ili hatimae na wewe uweze kupata wema.
Na katika kudumisha huo wema wengine wakasema deni la ikhsani hulipwa kwa ikhsani ikiwa na maana ya kwamba kamwe usikubali kwa mtu anaye kufanyia ikhsani ukamlipa nuksani (maovu).
Yote haya tumeyapigia mfano kwa kumlinganisha Dr. Mohammed Haji Shaali ambaye ni Mfanyakazi ya Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani tokea miaka ya 1990 ni takriban miaka 31 sasa. Na miaka yote hio alikuw aakitoa huduma kama mtaalamu wa mionzi katika hospitali hio. Mtu ambae ni Muhimu si kwa Hospitali ya Abda...