Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka Uongozi wa Wizara ya Afya kuongeza nguvu katika kitengo cha damu salama kwa kuwaongezea vitendea kazi watendaji wao pamoja na kujali stahiki zao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Mhe. Hemed alieleza hayo katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani, illiyofanyika katika Ofisi ya Benki ya uchangiaji damu Sebleni wilaya ya Mjini Unguja.
Aliwapongeza wafanyakazi wa kitengo hicho kwa kazi kubwa wanayofanya katika kijitoa kwao kwa moyo mmoja kwa kuhakikisha wanafikia lengo la ukushanyaji wa damu kwa wingi ili kuoka maisha ya watu wkiwemo mama wajawazito, watoto na watu waliopatwa na ajali.
Alisema kuwa kutokana na suala la uchangiaji damu kumgusa kila kila mmoja kat...