Monday, November 25

afya

Marekani Yaahidi Kuendeleza Mashirikiano na Zanzibar Katika Kuimarisha Afya ya Wananchi Wake.
afya

Marekani Yaahidi Kuendeleza Mashirikiano na Zanzibar Katika Kuimarisha Afya ya Wananchi Wake.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe.Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright alipofika Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar. Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright akiagana na Waziri Nassor Mazrui baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mnazimmoja. Picha na Makame Mshenga. Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar. Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright ameahidi Serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha afya za wananchi. Ameeleza kuridhishwa na hatua kubwa iliyofikiwa katika mapambano dhidi ya maradhi ya Maleria na kusema kuwa Marekani itaendeleza mkakati utakaohakikisha maradhi hayo ya...
KUELEKEA SIKU YA VIPIMO DUNIANI, TBS YAWATAKA WATUMIAJI WA VIPIMO VYA AFYA KUVIHAKIKI UBORA
afya, Biashara

KUELEKEA SIKU YA VIPIMO DUNIANI, TBS YAWATAKA WATUMIAJI WA VIPIMO VYA AFYA KUVIHAKIKI UBORA

Afisa vipimo Mwandamizi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Ramadhan Mfaume akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Siku ya Vipimo Duniani yenye kauli mbiu  “VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA”.  Mkuu wa Maabara ya Vipimo (TBS), Bw.Joseph Mahila (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Siku ya Vipimo Duniani yenye kauli mbiu  “VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA”. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO) ****************************** NA EMMANUEL MBATILO Kuelekea Siku ya Vipimo Duniani Mei 20,Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka watumiaji wa Vipimo katika sekta ya afya nchini kuhakikisha vipimo hivyo vimepitishwa na Shirika hilo kabla havijatumika. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Afisa Vipimo...
UN: Vifo 745,000 vimetokona na kufanya kazi sana
afya, Kimataifa

UN: Vifo 745,000 vimetokona na kufanya kazi sana

Utafiti wa Shirika la Afya duniani (WHO) na la Kazi duniani (ILO) unaonesha kufanya kazi kwa muda mwingi katika kipindi cha mwaka 2016, kumechangia vifo 745,000. Katika utafiti wao huo, mashirika WHO na ILO kwa pamoja yanakadiria watu 398,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa kiharusi na 347,000 magonjwa ya moyo kwa 2016. Sababu ambayo inaoneshwa ni kufanya kazi kwa muda mrefu kunakofikia masaa 55 kwa wiki. Kati ya mwaka 2000 na 2016, idadi ya vifo vilivyotokana na magonjwa ya moyo kwa sababu ya kufanya kazi kwa muda mrefu viliongezeka kwa asilimia 42, na kiharusu asilimia 19, na mzigo mkubwa wa vifo hivyo kwa asilimia 72 unabebwa na wanaume. Maeneo ambayo yanatajwa kuwa na athari zaidi  kwa wafanyakazi wa umri wa kati au wazee ni Magharibi mwa Asia Pasifiki na Ukanda wa Kusi...
ZFDA yateketeza Tani 14 za mchele aina ya mbea.
afya, Biashara

ZFDA yateketeza Tani 14 za mchele aina ya mbea.

NA ZUHURA JUMA, PEMBA JUMLA ya tani 14 za mchele aina ya mbea umeteketezwa katika kware ya Pujini Wilaya Chake Chake baada ya kuonekana kuwa haufai kwa matumizi ya binadamu. Akizungumza baada ya kumaliza zoezi la uteketezaji wa mchele huo, Mkurugenzi wa Wakala wa Chakula na Dawa (ZFDA) Pemba Nassir Salum Buheti alisema, mchele huo ulipatikana mwezi wa Febuari mwaka huu katika bandari ya Mkoani. Alisema kuwa, mchele huo uliokuwa kwenye meli ya Azam Silink ambao ulitokea Mkoani Tanga kuja Pemba na baada ya kufika ulikuwa tayari umesharoa. Alieleza kuwa, kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama waliuzuia mchele huo, kwani wangeuruhusu kuingia sokoni ni kuhatarisha maisha ya wananchi. “Mchele unaporoa kuna uwezekano mkubwa wa kuota wadudu, hivyo hauwezi kutumika ...