Monday, November 25

afya

Afariki dunia kwa kujinyoga huko Shengejuu.
afya, Kitaifa

Afariki dunia kwa kujinyoga huko Shengejuu.

NA ZUHURA JUMA, PEMBA   MTU mmoja amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba huko Shengejuu Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.   Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Sadi Khamis amemtaja aliyepatwa na mauti hayo kuwa ni kijana Abrahman Juma Mohammed (22) mkaazi wa Shengejuu Wilaya ya Wete.   Kamanda Sadi alifahamisha kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi  majira ya saa 3:45 huko Kijijini kwao Shengejuu.   Kamanda Sadi alieleza kuwa, kabla ya kupatwa na mauti hayo marehemu alikwenda nyumbani kwao baada ya kupata msaada wa vyakula na pesa taslimu shilingi 100,000/- ambavyo vitu hivyo vilitolewa msaada.   “Lakini baada ya kufika nyumbani kwao na kujiangalia vizuri ile baha...
Jamii Watakiwa Kuchukua Tahadhari na Mvua za Masika.
afya, Kitaifa

Jamii Watakiwa Kuchukua Tahadhari na Mvua za Masika.

        Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar. Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar imeitaka jamii kuchukuwa tahadhari juu ya mvua za masika  zinazoendelea kunyesha ili kuepukana na majanga ambayo yanaweza kujitokeza . Hayo yameelezwa na Mkuu wa Devisheni na Athari za  Mapema, Omar Ali Mohamed wakati wa kujadili mwelekeo wa mvua za masika katika Kikao cha Wadau wa Maafa kilichofanyika katika Ukumbi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Maruhubi . Alisema hali ya mvua inayoendelea kunyesha ni ya kiwango cha wastani vilevile ipo haja ya jamii kuchukua tahadhari kutokana na athari zinazoendelea kujitokeza katika maeneo mbali mbali. Alifahamisha kuwa madhara yanayoweza kujitokeza na kuleta athari katika maisha ya watu na mali zao ambayo yanato...
Shirika la Afya (WHO) limesema takriban nusu ya maambukizi ya Virusi vya Corona yaliyorekodiwa duniani wiki iliyopita ni kutokea Nchini India.
afya

Shirika la Afya (WHO) limesema takriban nusu ya maambukizi ya Virusi vya Corona yaliyorekodiwa duniani wiki iliyopita ni kutokea Nchini India.

WHO imesema India imerekodi 46% ya maambukizi ulimwenguni pamoja na 25% ya vifo vyote vilivyoripotiwa wiki iliyoisha. Katika saa 24 zilizopita, watu 3,780 katika Taifa hilo wamepoteza maisha. Waziri Mkuu, Narendra Modi na Serikali yake wamekosolewa kwa kutochukua hatua za kudhibiti wimbi la pili la mlipuko huo mapema. Matamasha ya Dini na mikusanyiko ya kisiasa iliyovutia maelfu ya watu imetajwa kuchangia maambukizi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Mpango Atembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa.
afya

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Mpango Atembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akimpa pole na kumfariji Bibi Leah Mahibwa (50) Mkazi wa Manyoni aliyelazwa kwa Matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, wakati Makamu wa Rais alipofika katika Hospitali hiyo leo Mei 04,2021. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akisalimiana na kuwapa pole Wananchi mbalimbali waliofika  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma kwa ajili ya kupatiwa Matibabu wakati Makamu wa Rais alipofika katika Hospitali hiyo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa mambo ya Neuron Surgery Dr. Humba, kuhusu maendeleo ya Matibabu ya Bibi Zaveria Chuga Malamba (62) Mkazi wa ...
Wamiliki wa Vituo vya Afya Binafsi Wapewa Wiki Moja Kukamilisha Taratibu za Usajili Vyenginevyo Vitafungiwa
afya

Wamiliki wa Vituo vya Afya Binafsi Wapewa Wiki Moja Kukamilisha Taratibu za Usajili Vyenginevyo Vitafungiwa

Meneja Masoko wa Kampuni ya Wide Spectrum LTD ya Dar es salaam Khamis Saleh Fakir akimkabidhi Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazurui msaada wa dawa kwa ajili ya vituo vya Afya vya Unguja, (kushoto) Mfamasia Mkuu Zanzibar Habib Ali Sharif. Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazurui akitoa tamko kwa wamiliki wa Hospitali binafsi kukamilisha taratibu za kisheria za kufanya shughuli zao za kutoa huduma. Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazurui akitoa tamko kwa wamiliki wa Hospitali binafsi kukamilisha taratibu za kisheria za kufanya shughuli zao za kutoa huduma. Baadhi ya wamiliki wa vituo vya afya binafsi wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika Wizarani Mnazimmoja. ...