Virusi vya corona: Mambo nane tuliojifunza ndani ya mwaka mmoja wa janga la corona
Wakati mtu wa kwanza aliyepata Covid-19 (Sars-CoV-2) ilipobainika mwaka mmoja uliopita, virusi hivyo viliwafanya wanasayansi, madaktari na wagonjwa kushindwa kuuelewa ugonjwa.
Mwaka mmoja sasa tangu janga hili litokee, limesababisha vifo vya watu zaidi ya milioni 2.6 na wengine milioni 117 kuambukizwa duniani kote.
Lakini katika wakati huu wote , madaktari na wanasayansi wamekuwa wakikusanya ushahidi wa namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 kuhusu virusi vipya vya corona - na sasa tunafahamu zaidi kuhusu ugonjwa huo na namna unavyoambukizwa, na namna utakavyoweza kutibiwa vyema.
Haya ni mambo nane ambayo tumejifunza kuhusu virusi vya corona:
1. Jinsi barakoa ilivyokuwa muhimu kujikinga na Covid-19
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
...