Sunday, November 24

afya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Amefika Hospital ya Mnani Mmoja Kuwafariji Majeruhi Waandishi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
afya, Kitaifa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Amefika Hospital ya Mnani Mmoja Kuwafariji Majeruhi Waandishi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

  arais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimfariji na kumpa pole Mpiga Picha wa Makamu wa Pili wa Rais Ndg. Hassan Issa, aliyelezwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, baada ya kupata ajali wakiwa katika msafara wakielekea Mkoa wa Kusini Unguja leo asubuhi. Rais Dk. Mwinyi alifika Hospitali kuu ya Rufaa ya MnaziMmoja kwa ajili ya kuwakagua majeruhi wa ajali ya gari iliyotokea asubuhi ya leo huko Kitogani, Mkoa wa Kusini Unguja ambayo imewahusisha wafanyakazi wa kitengo cha habari cha Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Akiwa ameongozana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Rais Dk. Mwinyi alipata fursa ya kuwakagua majeruhi hao waliopata ajali hiyo na kuwaombea kupona kwa harak...
Asasi za kiraia zatakiwa kushirikiana na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokomeza Kifua Kikuu.
afya

Asasi za kiraia zatakiwa kushirikiana na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokomeza Kifua Kikuu.

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA ASASI za kiraia kisiwani Pemba zimetakiwa kushirikiana pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa kifua kikuu ambao unaathiri jamii siku hadi siku. Akizungumza na wanachama kutoka asasi za kiraia pamoja na watu wa tiba asilia, katika Ukumbi wa Ofisi ya Ukimwi Machomane Chake Chake dk. Khamis Abubakar kutoka Kitengo Shirikishi Kifua kikuu, Homa ya ini, Ukimwi na Ukoma Zanzibar alisema, ushirikiano unahitajika katika kuhakikisha ugonjwa huo unamalizika. Alisema kuwa, kifua kikuu kipo ingawa wenye dalili hawafiki kwenye vituo vya tiba, hivyo kupitia asasi za kiraia pamoja na watu wa tiba asilia, washirikiane na Serikali kuwatafuta wagonjwa hao, jambo ambalo litasaidia kuwagundua mapema na kuzuia kuambukiza w...
Virusi vya corona: Je tunaweza kupata virusi vya corona kupitia macho?
afya

Virusi vya corona: Je tunaweza kupata virusi vya corona kupitia macho?

Daktari wa kwanza duniani kufariki dunia kwasababu ya ugonjwa wa Covid-19 alikuwa daktari bingwa wa macho Li Wenliang: na tangu wakati huo, macho yamekuwa yakihusishwa kwa karibu sana na janga la corona. Ingawa moja ya njia inayofahamika katika maambukizi ya ugonjowa wa corona ni matatizo katika mfumo wa kupumua, lakini pia unaweza kusambazwa miongoni mwa binadamu kwa mikono na kushika maeneo machafu. Lakini kisichofahamika ni virusi vinavyopatikana katika machozi ya binadamu pamoja, seli za konea na utando wa kamasi. Kupata maambukizi ya virusi vya corona kupitia macho na machozi ni jambo linalowezekana kabisa. Virusi vilivyopata maambukizi ya erosoli yaani umajimaji hukutana na eneo la jicho na baadaye huingia katika mfumo wa upumuaji kupitia...
Corona inaua zaidi wanaume kuliko wanawake Afrika
afya

Corona inaua zaidi wanaume kuliko wanawake Afrika

Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa virusi vya corona vinasababisha vifo kwa wanaume wengi zaidi barani Afrika kuliko wanawake ambao kwa sehemu kubwa waandamwa na uwezekano wa kupoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi kuliko Covid-19. Utafiti uliofanywa kwenye nchini 28 za Afrika, ikiwemo Guinea, Mauritius na Uganda umeonesha kwa wastani idadi ya wanawake waliopata maambukizi au kufa kwa corona ni ndogo ikilinganishwa na wanaume. Takwimu zilizokusanywa zinaonesha kwa wastani asilimia 41 ya wanawake barani Afrika ndiyo wamekumbwa na janga la corona lakini idadi hiyo inatofautiana miongoni mwa mataifa. Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika Matshidiso Moeti amesema kwa wanawake janga la covid-19 limesababisha ukosefu wa huduma za uzazi na wengi wanaweza ...
MHE. HEMED: SMZ INATAMBUA MCHANGO WA INDIA KATIKA HUDUMA ZA UTABIBU
afya

MHE. HEMED: SMZ INATAMBUA MCHANGO WA INDIA KATIKA HUDUMA ZA UTABIBU

  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na India katika  sekta ya Utabibu kwa kuimarisha Afya za wananchi wake. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameleza hayo wakati akizungumza na viongozi wa hospital ya SIMS ya India Afisni kwake Vuga jijini Zanzibar. Amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza ushirikiano wake na hospitali hiyo kutokana na matibabu mazuri yanayotolewa na madktari katika nyanja mbali mbali akitolea mfano magongwa ya moyo, saratani,tenzi dume na magonjwa mengineyo. Nae, Mkurugenzi Mkuu kutoka hospital ya SIMS Bw. Galal Ahmed Dawood amemshkuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa ushirikiano wanaopatiwa kutoka serikalini  tangu hospital yao ilipoanza kufanya kazi  zake. Kwa upand...