Sunday, November 24

afya

“SMZ ITAENDELEA KUUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YASARATANI” MHE.   HEMED
afya, Kitaifa

“SMZ ITAENDELEA KUUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YASARATANI” MHE. HEMED

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imezidi kuimarisha mipango yake ya udhibiti wa ongezeko na kupunguza athari zinazosababisha uwepo wa maradhi ya saratani Nchini ikilenga kulipa umuhimu mkubwa suala zima la Afya bora kwa Wananchi wake. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo Afisini kwake Vuga wakati akianzisha Rasmi hamasa na vugu vugu kuelekea ndani ya Wiki  ya maadhimisho ya Siku ya Saratani Ulimwenguni inayofikia kilele chake ifikapo Tarehe Nne Febuari ya kila Mwaka. Mheshimiwa Hemed Suleiman amewataka Wananachi, na Wataalamu ambao tayari wameshakuwa na uzoefu na mazoezi kama hayo wakaendelea kushajiisha wananchi kushiriki kwenye upimaji wa maradhi hayo linalotarajiwa kufanyika Hospitali ya Wete Pemba kuanzia asubuhi ya Tarehe Pi...
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo ;”TISHIO LA COVID-19 NI HALISI. VIONGOZI NA WANACHAMA TUCHUKUE TAHADHARI”.
afya, Kitaifa

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo ;”TISHIO LA COVID-19 NI HALISI. VIONGOZI NA WANACHAMA TUCHUKUE TAHADHARI”.

Maelekezo ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo kwa Viongozi na Wanachama kuhusu tahadhali dhidi ya tishio la mlipuko wa pili wa janga la Covid-19   Mwaka jana dunia ilikumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 unaosambazwa na virusi vya Corona. Tangu Januari 30, 2020 Shirika la Afya Duniani (WHO) lilipotangaza rasmi uwepo wa mlipuko wa virusi hivi, mataifa mengi yamepoteza mamia na maelfu ya watu kote ulimwenguni. Tanzania pia haijanusurika na dhahama hii. Kama ilivyo tabia ya majanga ya namna hii wakati wote ambao yamepata kutokea duniani, yamekuwa na kawaida ya kujirudia kwa awamu mbili. Hivi sasa, dunia inakabiliana na mlipuko wa awamu ya pili wa virusi vya Corona. Taarifa na takwimu za ongezeko la vifo vinavyotokana na janga hili kutoka maeneo na nchi mbalimbali k...
Msemaji  wa Serekali Dkt Abbas: Tanzania inazingatia tahadhari dhidi ya corona.
afya, Kitaifa

Msemaji wa Serekali Dkt Abbas: Tanzania inazingatia tahadhari dhidi ya corona.

Eagan Salla BBC Swahili, Dar es Salaam Msemaji mkuu wa serikali nchini Tanzania Dkt. Hassan Abbas amesema Tanzania inazingatia miongozo yote ya tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona na hata wakati huu ambao dunia inapambana na wimbi la pili la maambukizi ya virusi hivyo. Akihojiwa na kitoa cha redio cha EFM kilichopo jijini Dar es salam, Dkt. Abbas amesema “Sisi Tanzania msimamo wetu ni ule ule,tunafahamu tatizo lipo duniani na dunia inahangaika lakini cha kwanza watanzania waondoe hofu wizara ya afya ilishatoa miongozo, ile miongozo bado ipo haijawahi kufutwa kuna tahadhari za kuchukua hivi wewe kunawa mikono mpaka covid? Alihoji Dkt Abbas. ‘’ Tulikuwa tuna nawa sana shule baadaye tukaacha kwahiyo kuna zile tahadhari kama alivyosema juzi Mh Rais tuendelee kuzichukua lak...
Virusi vya corona: Maswali 4 ambayo hayajajibiwa kuhusu chanjo ya corona
afya, Kimataifa

Virusi vya corona: Maswali 4 ambayo hayajajibiwa kuhusu chanjo ya corona

Kukimbizana na muda. Hivi ndivyo tunavyoweza kuelezea uhamasishaji wa chanjo kwa wakazi wa dunia dhidi ya virusi vya corona na kurejesha hali ya kawaida kwa haraka iwezekanavyo. Hadi kufikia tarehe 23 Januari, zaidi ya watu milioni 60 walikuwa tayari wamepata baadhi ya dozi za chanjo dhidi ya virusi vya corona. Lakini kadri nchi zaidi zinavyoanza au kuharakisha kampeni, mambo kadhaa yanasalia kutofahamika . Bado haijawekwa wazi ni muda gani kinga ya chanjo inadumu baada ya kutolewa au kama aina mpya ya virusi ambayo imejitokeza kote duniani itakuwa sugu na kuifanya chanjo kutokuwa na ufanisi. Takriban miezi miwili baada ya mpango mkubwa wa utoaji wa chanjo ya watu wengi kwa mkupuo ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia, tunaangazia maswali yana...
35 wamefanyiwa upasuaji katika hospitali ya Chake Chake Pemba kwa  ugonjwa wa bawasili na kidole tumbo (appendix)
afya, Kitaifa

35 wamefanyiwa upasuaji katika hospitali ya Chake Chake Pemba kwa ugonjwa wa bawasili na kidole tumbo (appendix)

NA ZUHURA JUMA, PEMBA JUMLA ya wagonjwa 35 wamefanyiwa upasuaji katika hospitali ya Chake Chake Pemba baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa bawasili na kidole tumbo (appendix) kuanzia mwaka 2019 hadi mwaka 2020. Kati ya wagonjwa hao waliofanyiwa upasuaji wanawake ni 20 na wanaume ni 15. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi daktari Bingwa wa Upasuaji katika hospitali hiyo Yunus Pandu Buyu alisema, mwaka 2019 walifanyiwa upasuaji wagonjwa 19 na mwaka 2020 walifanyiwa wagonjwa 16. “Kati ya wagonjwa hawa 35, waliofanyiwa upasuaji kwa ugonjwa wa bawasili ni watu 13 na wagonjwa 22 walifanyiwa kwa ugonjwa wa kidole tumbo, ambapo wanawake waliofanyiwa upasuaji wa bawasili ni nane na kidole tumbo ni 12, wakati wanaume waliofanyiwa upasuaji wa bawasili ni watano na kidole tumbo ni ku...