Mukrim mohammed-Zanzibar
Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) limezindua mpango wake mpya wa kubadili muonekano na taswira yake kijamii na kibiashara hatua ambayo inalenga kuakisi ukuaji wa shirika hilo sambamba maboresho ya huduma zake kwa wateja.
Hatua hiyo mkakati inahusisha mfululizo wa mabadiliko chanya yanayohusisha muonekano mpya wa nembo ya shirika hilo, muonekano wa nyaraka rasmi za ofisi, maboresho ya huduma kwa wateja sambamba na mabadiliko ya muonekano wa ofisi za shirika hilo.
Hafla ya uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa ZIC imefanyika leo Zanzibar, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dkt. Saada Mkuya Salum. Pamoja na Waziri Mkuya pia walikuwepo Naibu Kamishna wa Bima Tanzania, Khadija Issa Said, Balozi wa Bima nchini Wanu Hafidh A...