Zaidi ya wakulima 3000 wanapokea fedha zao kupitia TigoPesa
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
WAKULIMA wa Zao la karafuu Kisiwani Pemba, wameshauriwa kuendelea kupokea fedha zao kwa kutumia TigoPesa, kufanya hivyo ni kuwasaidia vijana waliojiajiri wenyewe kuwa mawakala wa mitandano ya siku.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa TigoZantel Zanzibar Azizi Said Ali, wakati alipokua akizungumza katika hafla ya chakula cha mchana na utoaji wa zawadi, kwa wakulima wa zao la karafuu Kisiwani Pemba, hafla iliyofanyika Mjini Chake Chake.
Alisema wameamua kuwa karibu zaidi na wale wanaoshirikiana nao kwa kukubali kulipwa kutumia TigoPesa, kwani waliokubali kulipwa ni ndugu zao na wametoa sadaka kubwa kwa vijana waliojiajiri kupitia uwakala.
Alisema tokea mwaka huu kuanza msimu, zaidi ya wakulima 3439 wamelipwa fedha zao kupitia miamala ya TigoPesa, na kuw...