TRA yakabidhi bati uongozi wa skuli ya Michenzani Mkoani
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
MWENYEKITI wa Kamati ya Ujenzi ya Skuli ya Michenzani Hamud Malim Khami, ameushukuru uongozi wa TRA Mkoa wa kikodi Pemba, kwa kuwakabidhi bati 50 zenye thamani ya shilingi Milioni 1,740,000/ ikiwa ni utekelezaji wa ahadi kwa skuli hiyo.
Alisema kwa sasa wanahitaji bati zisizopungua 300, kwa ajili ya uwezekaji wa bweni la wanafunzi wakike, wakati watakapokua wanakabiliwa na mitihani yao ya taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa bati hizo, kutoka kwa watendaji wa TRA Mkoa wa kikodi Pemba, huko Chokocho Wilaya ya Mkoani, ikiwa ni Wiki ya Shukurani kwa mlipakodi Pemba, ilioambatana na kauli mbiu “Kodi Yetu, Maendeleo Yetu, Tuwajibike” yalyoandaliwa na TRA Pemba.
Alisema kwa sasa bweni hilo linakabiliwa na changam...