Taasisi ya Ifraj yakabidhi boti za uvuvi kwa vijana
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
TAASISI ya Ifraj Zanzibar Foundation imekabidhi boti tatu za uvuvi, kwa vijana wa Shehia za Mvumuni, Mfikiwa Wilaya ya Chake Chake na Mchakwe Wilaya Mkoani, ili ziweze kuwasaidia katika shughuli zao za uvuvi na kujiongezea kipato chao.
Akikabidhi boti hizo Mkurugenzi wa taasisi hiyo Pemba Abdalla Said Abdalla, alisema lengo kuu la Taasisi hiyo ni kusaidia vijana hao na kuwarahisishia kazi zao za uvuvi, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali ya Zanzibar katika dhana yake ya uchumi wa Buluu.
Hayo aliayeleza kwa nyakati tafauti wakati wa hafla ya kukabidhi boti hizo, pamoja na mashine zake kwa vijana hao ili kujishuhulisha na shuhuli zao za uvuvi.
Alisema sekta ya uvuvi ni moja ya sekta muhimu na inayomtoa kijana kwa haraka kuliko kazi n...