ZRA yasogeza huduma zake kwenye maonesho Chamanangwe
NA ABDI SULEIMAN,PEMBA
AFISA Tehama Kutoka Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Tamima Is-haka Mzee, amewataka wananchi Kisiwani Pemba kuyatumia maonesho ya siku ya Chakula Duniani, yanayoendelea katika viwanja vya Chamanangwe, ili kujifunza mambo mbalimbali hasa taasisi za kiserikali zinazosimamia mapato ya nchi.
Alisema wananchi wanapotembelea taasisi hizo, wataweza kufahamu jinsi gani wanahamasishwa kudai risiti za kieletroki pamoja na kufahamu elimu nzima ya kodi.
Afisa huyo aliyaeleza hayo, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, huko katika banda la Mamlaka hiyo kwenye maonesho ya siku ya Chakula Duniani yanayoendelea kwenye viwanja vya Chamanangwe Wilaya ya Wete.
Alisema jambo kubwa ambalo wamelisongeza zaidi katika maonesho hayo, ni uwepo wa mfumo wa kukusanyia...