PBZ yaazindua wiki ya huduma kwa wateja Pemba
NA ABDI SULEIMAN.
MKURUGENZI wa Biashara wa bank ya watu ya Zanzibar Eddie Mhina, amesema PBZ inathamini sana wateja wake, ndio maana wakawa wanafanya vitu tafauti tafauti katika kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kukirudisha kwa wananchi kile wanachokipata.
Alisema katika kutilia mkazo malengo yao ya kutoa huduma bora, imefungua kituo cha huduma kwa wateja kwa kutumia simu na mteja anaweza kupiga simu namba 0800000004, na kutatuliwa changamoto zake, pamoja na kuongeza vituo vipya, mawakala kila maeneo na ATM.
Mkurugenzi huyo aliyaekeza hayo, katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja wa bank hiyo, hafla iliyofanyika mjini Chake chake Mkoa wa kusini Pemba.
"Sisi kama benk wiki hii tutaiadhimisha mwezi mzima huu, katika kutoa huduma nzuri kwa ...