Kiwango cha madini ya uranium cha Iran kimepita mara 12 ya kiwango kinachohitajika, yasema IAEA
Shirika la Kimataifa la nishati ya atomiki (IAEA) limesema kuwa akiba ya uranium ya kiwango cha chini imefikia kilo 2,442.9 mwezi huu.
Iran inasisitiza kuwa mipango yake ya nyuklia ni ya malengo ya amani tu. IAEA pia ilisema kuwa maelezo ya Iran kwa ajili ya uwepo wa nyuklia katika eneo ambalo haijalitangaza wazi ''sio ya kuaminika''
Kwenye ujumbe wa Twitter, balozi wa Iran katika IAEA, Gharib Abadi, alisema kuwa "kauli zozote za haraka zinapaswa kuepukwa", akiongeza kuwa: "mazungumzo yanaendelea kwa lengo la kukamilisha azimio la suala hilo ."
Katika ripoti yake ya hivi karibuni, iliyosambazwa kwa wanachama, IAEA kutambua eneo ambako ilipata vifaa vya nyuklia.
Chanzo ambacho hakikutajwa kililiambia shirika la habari la AFP kwamba hapakuwa na kiashiria chochote kwamba h...